.

.
Wednesday, April 9, 2014

10:07 PM
 Na Bertha Ismail-Arusha

Waandaji wa mbio za Sokoine mini Marathon kwa mwaka huu kwa ajili Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, marehemu Edward Sokoine, wamezifanyia mbio hizo mabadiliko.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa, Mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema mabadiliko hayo yanatokana na maombi mbalimbali ya washiriki wa mbio hizo.

Alisema kuwa madai hayo ya msingi ni kutokana na msimu huu kuwepo kwa ratiba iliyobanana ya mashindano ya kitaifa na ya kimataifa ikiwemo Ngorongoro half Marathon ya Tigo inayotarajiwa kufanyika april 9 mwaka huu.

"Tunaomba radhi kwa kufanya mabadiliko ya ghafla! Hiyo ni kutokana na mashauriano kati yetu sisi waandaaji, Chama cha Riadha Mkoa na wanariadha wenyewe”

“Pia imeamuliwa kwamba siyo vizuri kuwakimbiza wanariadha mbio ndefu mara mbili kwa wiki moja, sababu pia kutakuwa na
Tigo Ngorongoro Half Marathon Aprili 19, mwaka huu," alisema Gidabuday.

Aidha, Gidabuday kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya mbio hizo inaishukuru familia ya hayati Sokoine kwa kubariki mabadiliko hayo na kuongeza kuwa, uamuzi huo mgumu umetokana na moyo wa kizalendo.

Alisema kuwa pamoja na mbio hizo za kitaifa, pia  kuna wanariadha watakaoshiriki ambao ratiba inaonesha kuwa watakuwa na mbio za kimataifa nchini China mapema mwezi ujao.

"Tuishukuru Familia ya Sokoine kwa moyo wa kizalendo zaidi kwa ,kuridhia ombi letu na pia imekuwa wazo zuri kwa wanariadha wazoefu ambao wanafahamu athari za kukimbia mbio ndefu mfululizo”

Alisema kuwa pia wazo hilo litakuwa faida kwa wananchi wengi sasa kuweza kushiriki kilomita 10, kutokana na wale wa mbio hizo kukimbia kilomita chache" alisema Gidabuday.

Aidha gidabuday alisema kuwa taratibu zingine hadi sasa zipo kama
zilivyopangwa, ambapo zoezi la kujisajili linaendelea Uwanja wa
Sheikh Amri Abeid Karume kwa sh 2,000 tu kwa wale watakaopenda kuungana na watanzania wenzao kumuenzi Hayati Sokoine kwa mbio hizo.

0 comments:

Post a Comment