Na Bertha Mollel
WATU
zaidi ya 50 wamenusurika kufa mara baada
ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu lililotengenezwa kwa mkono kulipuka na
kuwajeruhi vibaya watu 15 sehem
mbalimbali za mwili katika bar ya Arusha
Night Park iliyopo maeneo ya mianzini mjini hapa.
Watu
hao walijeruhiwa vibaya na mlipuko huo
mapema jana, april 13 majira 1;30 jioni mara
baada ya watu hao waliokuwa wakipumzika
katika baa hiyo kwa lengo la kuangalia
mpira kukusanyika.
Akizungumza
baada ya kutembea eneo la tukio na kutembelea
majeruhi hao katika hosipitali ya Selian, na
Mount meru mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa tukio hilo
limetokea bila kuwepo kwa mitazamio yeyote hivyo kuwataka wananchi wawache vyombo vya dola kufanya kazi yao ya
uchunguzi.
Mulongo
alieleza kuwa katika tukio hilo watu walikuwa wanaendelea na kazi zao na ndipo
mara waliposikia kitu kama kishindo na ghafla ndipo watu hao walipoanza
kurupushani za hapa na pale kutokana na mlipuko huo wa bom.
Alisema
kuwa, baada ya tukio hilo polisi walifika eneo la tukio na
kuwachukua majeruhi hao na kuwapelekea katika hospitali ya Mount Meru, Selian,
na hospitali ya st.elizabeth, pamoja na mount meru kwa ajili ya kupata
matibabu.
Aidha
kati ya majeruhi hao 15, watatu walitibiwa na kuruhusiwa ambapo 12 wanaendelea na matibabu huku wawili kati
yao akiwa na majeraha makubwa kwenye miguu ambaye alikuwa karibu na eneo bomu
lililopotegeshewa .
Aidha
Mkuu wa mkoa wa Arusha alitoa rai kwa watanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi pale wanapokuwa na taarifa za mtu yeyote kuhusika na tukio hilo hali
ambayo imekuwa ikitishia amani kutokana na tukio hilo kujirudia rudia.
Mulongo
alisema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea kupitia kamera zilizokuwa zimefungwa
kwenye bar hiyo katika kuwatambua wale wote waliohusika na tukio ambapo hatua
kali zitachukuliwa dhidi yao.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Mount Meru , mhudumu Luis John
alisema kuwa, alishtukia kishindo na moshi mkubwa wakati akihudumia wateja na watu kukimbia bila mwelekeo.
Aidha
alisema kuwa , bomu hilo linaonekana lilikuwa limetegwa ndani ya bar hiyo ambapo asilimia kubwa ya
wateja walikuwa wakiangalia mpira na ndio wengi wao waliojeruhiwa kutokana na
bomu hilo ambapo walianza kukimbia kimbia.
Alisema
kuwa hasara waliyoipata baada ya mlipuko huo ni baadhi ya wateja walikuwa
wameshahudumiwa walikimbia na bili huku wengine wakipoteza simu zao.
Wahudum wengine wa bar hiyo waliojeruhiwa ni Suzan John, Joyce
William, na Meneja wa bar hiyo aliyetambulika kwa jina la Halima .
Hata
hivyo hivyo baadhi wa wananchi wakizungumzia tukio hilo walisema kuwa matukio
ya kulipuka kwa mabomu mkoani Arusha yamekuwa yakitokea mara kwa mara na
kusababisha kuwepo kwa hofu kubwa miongoni mwa wananchi hasa ikizingatiwa mengi
yao kupigwa sehem zenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Mwananachi
huyo aliyejitambulisha kwa jina la ,Ashura Salimu mkazi Soweto alisema kuwa,
matukio hayo yamekuwa yakiwafanya kuishi kwa wasiwasi mkubwa ,kwani yamekuwa
yakijirudia mara kwa mara huku viongozi wa mkoa na Rais Kiwete wakitoa matamko
ya kuwasaka hadi kuwapata na kuwachukulia hatua za kisheria lakini matokeo yake
huishia hewani.
“Kama
unavyotambua hili si tukio la kwanza kutokea hapa Arusha, yametokea mabom mengi
tu ikiwemo la uwanjani hapa Soweto na lile la kanisani lililigharimu maisha ya
watu ambapo mbali na serikali ya mkoa kufika na kulitokea tamko lakini pia Rais
Kikwete alitoa tamko la kuwasaka na
kuhakikisha wanapatikana na kuchukuliwa hatua lakini kwa matokeo yake walitupa
taarifa kuwa wahusika wamewapata na wanawajua hivyo watawachukulia hatua kali
za kisheria, lakini maneno hayo baadae yalikuja kuonekena na kuungwa ungwa
kutokana na watu hao hawakutajwa majina kwa madai kuharibu upelelezi lakini pia
hatuwajui hadi leo na hakuna hatua waliochukuliwa”
Hivyo
aliomba serikali kuhakikisha kuwa inakuwa makini na kuchukua hatua za haraka
kwa watu hao ambao wamekuwa wakihusika na matukio hayo kwani kwa mkoa wa Arusha
imekuwa ikizua wasiwasi mkubwa badala ya
kuunga unga maneno wakati matukio hayo yanagharimu maisha ya watanzania.
Aidha
itakumbukwa kuwa hili ni bomu la nne kurushwa kwenye mikusanyiko ya watu ambapo
bomu la kwanza lilirushwa katika kanisa la katoliki la Joseph Mfanyakazi
liilopo olasiti katika uzinduzi wa
kanisa hilo, huku tukio la pili lilirushwa katika viwanja vya Soweto katika
mkutano wa kufunga kampeni za chadema , na la tatu likirushwa katika mkesha wa
mwaka mpya katika kanisa katoliki usa river .
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment