na Bertha mollel -Arusha
Kamati ya Olympic Tanzania (TOC)
imeahidi kuwapa Shirikisho la mchezo wa tae kwon do Tanzania TTF wataalmu na
wakufunzi wa mchezo huo toka korea na japani ukiwa ni mkakati wa kukuza
na kuendeleza mchezo huo wa kupigana karate ya kutukia mikono na mateke.
Rais wa TTF Ally Ramudh akizungumza
na Tanzania Daima mkoani hapa alisema kuwa kamati hiyo ya TOC imeona
jinsi Tanzania tulivyo na juhudi za mchezo huo ingawa hatujui utaalam wake sana
hali iliyowavutia na kuahidi kuleta wataalam watakaotuwezesha kujua
zaidi.
Alisema mpango huo unaodhaminiwa na
kamati ya Olypic ya kimataifa (IOC) umetokana na mafanikio ya kukubalika kwa
mchezo huo ambao kwa mara ya kwanza utatoa wawakilishi wa Tanzania katika
mashindano yajayo ya Olympic.
Kwa mujibu wa Ramudh wataalam hao
wanatarajiwa kutua nchini mwanzoni mwa mwezi wa sita, watazunguka Tanzania
nzima kufundisha na kuhamasisha mchezo wa tae kwon do ambapo asili yake ni
nchini korea na hong kong.
Akizungumzia juu ya mchezo huo Rais
huyo wa TTF alisema kwa sasa mchezo huo umekubalika na kukua kwa kasi kwani
sasa unafundishwa katika taasisi mbalimbali za kiusalama kama makampuni ya
ulizi na hata katika majehi ya ulinzi na usalama ikiwemo katika majeshi yetu ya
polisi.
Tae kwo ndo ni mcheza wa kujilinda
kwa kushambulia kwa kutumia mikono na miguu na umejijengea umaarufu mkubwa kwa
kuwawezesha mchezaji wa mchezo huu kujilinda hata akishambuliwa na kundi la
watu wenye silaha.
Mchezo huo wa Tae kwo ndo ni jamii
ya michezo ya karate ,kong fu na kick boxing wenye asili ya china,korea
na japan ambapo humwezesha mtu pia kuwa m’bunifu katika kujihami ambao pia
huleta burudani katika kuucheza na kuungalia watu wakiucheza.
0 comments:
Post a Comment