.

.
Wednesday, January 7, 2015

Na Bertha Ismail - Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Nyirembe Munassa Sabi amewataka wachezaji wa hapa mkoani Arusha kucheza soka kwa upeo wa kulipwa zaidi kuliko kuchukulia kama mazoezi au kujifurahisha ili kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa za kimataifa na kupatia fedha kupitia michezo.

Mkuu huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wachezaji wa timu nane zilizoshiriki mashindano ya ndondo yaliyojulikana kama “vipaji cup” vilivyofanyika katika uwanja wa Ilboru vilivyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha ambapo small galilaya fc ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe  hilo.

“Wachezaji wengi wa Tanzania pamoja na kucheza mpira na wengine kutumikia vipaji vyao vya soka lakini hawana upeo wa kuona kama mpira ni ajira bali wengi wao wanacheza kupata umaarufu hali ambayo haiwasaidii bali chezeni kwa kuwa na upeo wa kucheza soka la kulipwa kwani hapo ndipo utaweza kuweka nguvu zako kubwa kucheza vema na hatimaye kuwa kama ajira yako na kuitangaza nchi kimataifa”

“Tunajua hali ya nchi yetu na viongozi wenu wa soka bado hawajaweka mikakati mizuri Ya kuhakikisha wachezaji wa nchi hii wanafaidika na michezo ndio maana mnakata tamaa lakini kwa wenzetu wa nchi za nje mtu anaechezea hata ligi daraja la tatu analipwa na wanafanya usajili wa vipaji bora lakini hapa kwetu mchezaji anaetambulika ni hadi ligi kuu na kuika huko si leo mtakuwa mmesota sana, hivyo ninyi jitahidini kucheza kwa upeo wa kimataifa mtapata nafasi ya kucheza katika nchi hizo mlipwe vema” alisema mkuu huyo

Alisema kuwa wachezaji wa ligi za ngazi za chini hawalipwi hapa nchini kutokana na viongozi wa soka kutokuwa na upeo wa kuzitautia ligi hizi ufadhili wa kuzidhamini hali ambayo ukata huo huwafikia hadi wachezaji na kucheza soka lisilo na viwango kutokana na wengi wao kuwaza majukumu yao na umasikini hali ambayo wengi huamua kuacha kucheza soka kukabiliana na hali ya maisha na vipaji vyao kupotea.

Mashindano hayo ya vipaji cup yaliyoandaliwa na mwalim Joseph Zephania Laizer yalishirikisha timu nane za wilayani humo ikiwemo small galilaya, Red star, enterspot fc, moivo, red star, nature united,  kiurei, minara mitatu, na Ilboru ambapo mshindi wa kwanza small galilaya alitwaa kombe la fedha taslim shilingi laki moja, mshindi wa pili ikichukuliwa na red star na kufanikiwa kuzawadiwa fedha taslim 50,000 na mshindi wa tatu enterspot na kupatiwa 30,000.

Mwisho…..

0 comments:

Post a Comment