.

.
Saturday, January 31, 2015
Mlinda mlango wa Oljoro dihe makonga (Wa pili kushoto)  akiwa na kikosi chake hicho


Arusha

Mlinda mlango namba moja wa timu ya Maafande ya Jkt Oljoro yenye makazi yake jijini Arusha Dihe Hassani Makonga amujikuta akiitamani nafasi ya siku moja kuitumikia club ya Azam kama goli kipa wa timu hiyo.

Akizungumza na gazeti hili Makonga alisema kuwa pamoja na kuitumikia club ya Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza kundi B’ kwa sasa lakini matarajio yake makubwa ambayo amekuwa akiota kila kukicha ni siku moja kujikuta akitumia club ya Azam ambayo imekuwa ikiwajali sana wanamichezo wake pia kuwa na kituo kizuri cha soka.

“Mimi kwa sasa ndoto yangu kubwa ni siku moja kutumikia club ya Azam hivyo kwa sasa ninapambana kuhakikisha naipandisha oljoro kwa hali na mali ambapo nimekuwa nafanya  mazoezi yangu hata mda wa ziada kuhakikisha malengo yangu yanatimia ili kuwatendea haki, najua nitapata sifa ya kunisaidia kuitumikia club ya ndoto zangu” alisisitiza Makonga

“Unajua mimi tangu mdogo napenda mpira na namshukuru sana kocha wangu aliyenianzishia safari ya kutimiza ndoto zangu za kuwa mwanasoka wan chi hii kama mlinda mlango ambae ni Chalse Boniface Mkwasa kwa kunianzishia hili na mimi kuitendea haki leo na nitajivunia sana katika maisha yangu kuipandisha oljoro ambayo nikiwa ligi kuu itakuwa nafasi nzuri kwangu hivyo niwashauri na wachezaji wenzangu wanaoota siku moja kutumikia club kubwa wajitume sana waachane na starehe ili wafanikiwe”

Dihe makonga ambae ni mlinda mlango chipukizi, kwa mara ya kwanza anaitumikia club kubwa ya ligi daraja la kwanza lakini amekuwa na mafanikio makubwa sana katika timu hiyo hasa baada ya kuwa tegemezi na kufanikiwa kuwa kikosi cha kwanza huku akikubalika sana na wachezaji wanzake na mashabiki wa mkoa huu kummuamini hasa akiwa mlangoni katika michuano yoyote anaposimama langoni.

mwisho

0 comments:

Post a Comment