.

.
Saturday, January 31, 2015

Katika matukio niliyofuatilia na mwisho wa siku nikalia kama mtoto mdogo
 baada ya kushindwa kutetea haki ya muhusika,  baada ya kufa 
ni pamoja na hili, lililomhusisha mtoto wa kike
mwenye umri wa miaka mitano, amefariki duniani huko mkoani
Kilimanjaro, baada ya kubakwa na babake mzazi.
 
unajua ilikuwje?
 
  mtoto huyo alifanyiwa unyama na
babake aitwae Elisha Wazaeli, (38), huko Mang’ola, wilaya ya Karatu,
mkoani Arusha.
 
Kifo cha mtoto huyu ambacho kimewasikitisha watu wengi, kilitokea
Juni 4, mwaka 2014 katika hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi,
alikokuwa akipata matibabu.
 
mazingira ya tukio hadi kufikia kifo cha mtoto huyo, kwa taarifa za
 awali zilizotolewa kwa jeshi la
polisi zinaonyesha ya kuwa mtuhumiwa alisafiri na mtoto wake huyo hadi
Karatu  eneo alilomfanyia unyama huo.
 
“Alikaa na mtoto huyo huko Karatu kwa siku nne na baada ya kumfanyia
unyama huo, alirudi na mtoto huyo hadi Ngaramtoni, Arusha wanakoishi
lakini baba huyo alitofautiana na mama wa mtoto huyo kabla ya mama
huyo kumchukua mtoto na kwenda nae eneo la Kahe, Moshi, Vijijini, Mkoa
wa Kilimanjaro na wakati akisafiri na mwanae huyo
kwenda Mang’ola alimwacha mkewe Arusha Mjini.
 
baada ya kufika Kahe mtoto huyo alianza kuugua na
alipopelekwa katika hospitali ya TPC aligundulika anaumwa homa ya
matumbo na kupatiwa tiba na dawa lakini pamoja na tiba hiyo bado
alikuwa akisumbuliwa na maradhi.
 
Mama yake alipomchunguza zaidi aliambiwa na mtoto huyo ya kuwa
anaumwa na sehemu zake za siri na alipomhoji zaidi ndipo alipomwambia
ya kuwa babake alimuingilia kimwili wakiwa Karatu,ambapo  mamake
alimchunguza sehemu zake za siri na kukuta ameharibika vibaya  huku
akitoa harufu mbaya
 
mama huyo alitoa taarifa kwa jeshi la polisi ambapo maofisa wa
jeshi hilo walimchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitali ya Mawenzi
kwa uchunguzi zaidi na matibabu hadi alipofariki dunia juzi.
 
Ukweli ni kwamba mtoto Yule alipopelekwa polisi  Juni 4
alikuwa ameharibika vibaya sehemu zake za siri,kwani alikuwa akitoa
harufu ya kuoza,na baada ya kufika, alipelekwa hospitali ya
Mawenzi kwa ajili ya matibabu ambapo alilazwa,lakini alifariki dunia
ilipofika saa Moja usiku 
 
Hata hivyo baada ya mtuhumiwa kugundua swala hilo, limefika 
katika vyombo vya  sheria alikimbia.

wito wangu, wazazi jamani chonde chonde waleeni watoto wenu vema 
nikimaanisha muwe karibu nao hata lisaa kwa siku na kuzungumza nao
 kama kuna tatizo itakuwa rahisi kukuambia hasa hasa mama
pia wakagueni watoto wenu mara mara kwa mara sehem za siri
 msisubiri aoze kama huyu kwani angegundua mapema mwanae anaumwa 
angemuwaishia tiba na kifo hicho kisingemkuta malaika huyu

Mungu ailaze roho ya mwanamwali wake mahala pema peponi

0 comments:

Post a Comment