.

.
Tuesday, February 3, 2015

2:58 AM
mashindano ya riadha kwa ajili ya kuchagua timu mkoa yaliyohusisha wanaume 19 katika umbali wa kilimita 12 wakikatiza katika viwanja vya magereza vilivyoko kisongo jijini Arusha ambapo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Fabian Nelson


na Bertha Ismail - Arusha

Wanariadha Fabian Nelson na Catherine Lange wamefanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa miongoni wa wanariadha watakaotumika kuunda timu ya Taifa itakayowakilisha nchi katika mashindano ya Dunia hapo mwezi march mwaka huu Beijin nchini China.

Wanariadha hao wameonyesha uwezo wao wa kukata upepo mkoani Arusha kwenye mashindano ya wazi ya wanariadha kutoka mikoa ya Kanda ya kaskazini lengo ikiwa ni kujipima uwezo wa kushiriki mashindano ya Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Arusha February 21 mwaka huu.

Fabian Nelson akiwa miongoni mwa wanaume 19 walioshiriki mbio za kilomita 12 alishika nafasi ya kwanza kwa kumaliza kwa kutumia dakika 34:54:31 akifuatiwa kwa karibu na Gabriel Gerald kwa kutumia dakika 35:23:77 huku Uwezo Lukinga akiwa nafasi ya tatu kwa kutumia dakika 35:39:36.

Wasichana nane walikimbia umbali wa kilomita nane ambapo Catherine Lange  alikaa mbelena kuwa namba moja kwa kutumia mda wa dakika 27:27:05, akifuatiwa kwa karibu na Magdalena Crispine aliyetumia dakika 27:39:17 na namba tatu akiwa ni Anjelina Tsere aliyetumia dakika 28:43:96 kumaliza mbio zake.

Katika mbio hizo wako wanaume 20 pia walioshiriki mbio za kilomita nane ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Josephat Joshua kwa kutumia dakika 23:44:84 akifuatiwa na Tumaini Habiye aliyetumia dakika 24:31:53 na namba tatu alikwenda kwa Yohana Elisante kwa kutumia dakika 24:36:58.

Mashindano hayo ya wazi pia yalishirikisha wanafunzi waliokimbia umbali wa kilomita sita na Amina Mohamed aliwaacha wenzake na kuwa namba moja kwa kutumia dakika 23:12:93 akifuatiwa na Neema Kisuda kwa kutumia dakika 24:12:33 huku namba tatu ikichukuliwa na Yasmini Yusuph kwa kutumia dakika 27:59:33.

Akizungumzia mashindano hayo katibu wa chama cha riadha mkoa wa Arusha Alfredo Shahanga alisema kuwa lengo la mashindano hayo ya kanda ni kuangalia uwezo wa wanariadha hao na kuweza kuwapa nafasi ya kuunda timu itakayowakilisha mikoa hii kwenye mashindano ya kitaifa kama mwanzo wa safari ya kuelekea mashindano ya Dunia.

“Tumefanya haya mashindano kuangalia uwezo wa wanariadha wetu na tuchague watakaoweza kuunda timu ya mkoa ili watuwakilishe kwenye mashindano ya riadha ya kitaifa yanayoratibiwa na kamati ya riadha Taifa ambayo yamepangwa kufanyika February 21 hapa hapa Arusha”

“Mashindano hayo ya kitaifa yatachagua timu nzuri ya riadha Taifa itakayokuwa inajifua tayari kwenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia march 23 huko Beijin Nchini China, baada ya kufanyiwa mchujo wa kuridhisha lengo ikiwa mwaka huu tupate ushindi siyo kusindikiza kila mwaka” alisema Shahanga.

Mwisho,………..
  
   .  

0 comments:

Post a Comment