.

.
Wednesday, February 25, 2015

3:03 AM
Arusha

Chama cha Taekwondo mkoa wa Arusha imeamua kuingia katika shule za sekondari kusaka vipaji vipya vya mchezo huo lengo ikiwa ni kuongeza nguvu na kasi ya mchezo huo mkoani hapa ikiwa na maandalizi ya mapema ya timu bora itakayowakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpic hapo baadae.

Akizungumza na gazeti hili kocha wa timu ya Taekwondo Arusha Richard Kitolo alisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona mchezo huo unadumaa mkoani hapa kutokana na kukosekana kwa vipaji vipya vya vijana wenye vipaji na mchezo huo.

“Tumeamu kuingia mashuleni kutafuta vipaji vipya vya mchezo wa Taekwondo ikiwa ni kama maandalizi ya kushinda mashindano ya olilpiki hapo baadae hivyo kutokana na kukosekana kwa vipaji vipya tumeingia mashuleni na tumeanza na shule ya sekondari Braeburn na edmundi rise”

Kocha huyo ambae ni mmiliki wa Club ya Triple A’ taekwondo alisema kuwa wamekuwa na uhaba mkubwa wa wachezaji wa mchezo huo hasa mkoani Arusha hivyo wameamua kutafuta wenyewe katika shule za sekondari kote mkoani hapa wakisaidiana na walimu mbalimbali lengo ikiwa ni kufanya makali ya mchezo huo kutisha kimatifa hapo baadea

‘Unajua kwa sasa wanafunzi wa shule za sekondari ndio wenye uwezo mkubwa wa kuonyesha uwezo wa vipaji vyao hivyo tumeamua kujikita huko na tunaomba walimu waturuhusu kuwafundisha wanafunzi wao mchezo huo kwani mbali na mazoezi ya kujilinda lakini pia inawafanya wawe na akili kutokana na mazoezi pia tunawafundisha nidhamu”

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wa wananfunzi hao kuwaruhusu kutoa mazoezi hayo mda wa jioni kwa watoto wao kwani mbali na kuwa na uwezo wa kujilinda lakini pia itawasaidia watoto wao kupata ajira hapo baadae endapo watafanya vizuri

mwishooooo

0 comments:

Post a Comment