.

.
Friday, February 13, 2015Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya jumuia ya vijana wa chama cha wananchi CUF yaliyokuwa yafanyike Feb 13 mwaka huu.

Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari amesema .
 
hata hivyo licha ya jeshi la polisi kupiga marufuku maandamano hayo vijana hao wamesisitiza kuwa maandamano yao ya kuitaka tume ya uchaguzi kuongeza siku za kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura yanayotarajiwa kufanyika Feb 13 yako palepale.
 
Mwenyekiti wa JUVICUF taifa Bw Hamidu Bobali ameyasema hayo jijini Dar es Salaam ambapo amesema maandamano yao mbali na kuishinikiza tume kuongeza siku za kujiandikisha pia yana lengo la kulani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi nchini na kuongeza kuwa hawawezi kusitisha kutokana na hoja wanazotaka kuwasilisha zina maslahi mapana kwa taifa.

0 comments:

Post a Comment