.

.
Wednesday, February 11, 2015

3:18 AM
Katibu mkuu wa chama cha waigizaji nchini Twiza Mbarouk amewaonya wasanii wa kike kuacha kutumia miili yao vibaya kwa kujirahisi kingono ili kupata umaarufu utakaopelekea kujiongezea kipato badala yake wafanye kazi za sanaa kwa ubora itakayojiuza sokoni.

Mbarouk  aliyasema hayo jijini Arusha kwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa chama cha waigizaji mkoani hapa iliyohudhuriwa na wanachama zaidi ya 50 wanaotengeneza filamu mbalimbali na kusambaza nchini.

“Kwa sasa jamani mabinti ifikie mahali mseme basi kujidhalilisha wenyewe kwa kutumia miili yenu kujipatia umaarufu  utakaozalisha pesa badala yake tungeni na fanyeni kazi nzuri itakayouzika sokoni kwani kwa njia hiyo umaarufu huja wenyewe na kipato vilavile kuliko kutumika miili yenu”

“Mimi niwaambie tu umaarufu wa ngono haudumu hata siku moja kwani magonjwa nayo hayakai mbali na wewe pia unaweza ukajirahisi upate umaarufu na usipate lakini ukifanya kazi nzuri itakupa umaarufu mzuri utakaodumu na usio na majuto wala mateso pia kipato kitakuwa mara dufu”


Mbali na hilo aliwataka wasanii kutumia nafasi walizonazo kujiendeleza kielim ili kuweza kufanya kazi nzuri zitakazokwenda na wakati sokoni sambamba na kuimarisha vyama vyao vya sanaa ili kupata maendeleo zaidi kuliko kutumia mda mwingi kusambaratisha umoja wao.

Kwa upande wake mwenyekiti aliyepita bila kupingwa Fredy Elifas alisema kuwa kazi kubwa kwa sasa ya kufanya ni kuongeza wanachama kutoa 80 waliopo hadi 200 katika mwisho wa uongozi wake lengo ikiwa ni kuongeza nguvu katika chama hicho.

“Mbali na kuongeza nguvu lakini ni ili wanachama tunufaike na SACCOS watakayoianzisha ili kuacha kutegemea chanzo kimoja cha mapato pekee ambacho hakitawalipa wao na maisha yao ya baadae bali wawe na miradi itakayoendeshwa kwa fedha za mikopo watakazopata kutoka katika taasisi mbali mbali za kifedha”.

0 comments:

Post a Comment