.

.
Wednesday, February 11, 2015

3:16 AM

Mashidano ya kimataifa ya mpira wa miguu kwa vijana chini ya umri wa miaka 15 (Rolling store) yanayoshirikisha nchi za ukanda wa maziwa makuu yamehairishwa kwa mwaka huu kufuatia kuwepo na maswala ya uchaguzi pamoja na kura za katiba mpya.

Mashindano ya Rolling store yenye makao yake makuu mkoani Arusha, na kufanyika kila mwaka hapa nchini kwa kuwaalika nchi za ukanda wa maziwa makuu kushindana kisoka yamehairishwa kutokana na kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa maraisi na wabunge huku pia kukiwa na mchakato wa kupiga kura za maoni.

Akizungumza na gazeti hili, mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Rolling store, Ally Mtimwa alisema kuwa makao makuu ya taasisi hiyo yako Tanzania hivyo kutokana na kuwepo na shughuli maalum ya kiserikali kwa mwaka huu wameamua kupisha shughuli hiyo kama kuipa heshima nchi katika shughuli zake.

“Mashindano ya rolling store kwa mwaka huu hakuna kutokana na kuwepo kwa shughuli za uchaguzi na pia ni mwaka wa katiba ambapo kutakuwa na vuguvugu la kisiasa pia misukosuko ya kiuchaguzi hivyo na sisi kama wadau wa nchi hii hatuwezi kuingilia ratiba hiyo kwani hatuwezi kuwaalika wadau waje kushindana kindi nchi iko na shughuli maalum”

“Mbali na hilo pia hatufanyi mashindano kutokana na mikakati mipya tunayotaka kuanza ikiwemo kufanya mashindano kwa kuvuka mwaka mmoja mfano tukifanya mwaka huu hatufanyi mwaka kesho hii yote ikiwa ni kuyaboresha mashindano yetu pia kupata mda wa kufanya tathmini yetu juu ya mashindano yaliyopita”

Mtumwa alitumia nafasi hiyo pia kuwataka wadau wa soka wa mashindano hayo kujiandikisha kuwa wenyeji wa mashindano hayo katika nchi mbali mbali kwa mfumo huo mpya sambamba na kuwakaribisha wadhamini kujitangaza kupitia mashindano hayo ya kimataifa

“Mimi niseme tu kuwa kutokana na kuboreka kwa mashindano haya na kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu kwa sasa tunakaribisha nchi zingine sasa kuwa wenyeji wa mashindano haya kwa miaka ijayo pia wadhamini watumie fursa hiyo kujitangaza kwani hadi sasa hatuna wadhamini wakuu wa mashindano haya kwani kwa mwaka jana tulikuwa na wadhamini ambao ni Azam tv hivyo wengine wajitokeze” alisema Mtumwa.


mwisho...................

0 comments:

Post a Comment