.

.
Tuesday, February 3, 2015

3:24 AM
Monu Singh akipokea zawadi ya ushindi kutoka kwa kaptein wa timu ya Gkmkana Golf club, Robby Chadha
Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Taifa wa mchezo wa Hocky nchini kwa zaidi ya miaka 10 amefanikiwa kutwaa ushindi wa jumla wa mchezo wa gofu katika mashindano ya mwezi wa kwanza wa kuwania  vikombe vya Gupta (Gupta golf January monthly Mug) yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkana jijini Arusha.

Monu Singh amefanikiwa kutwaa ushindi wa jumla wa mashindano hayo yaliyodhamini wa campuni ya ya Gupta outo spare yalishirikisha jumla ya wanamichezo wa gofu 40 kwa kupiga mikwaju 66 katika mizunguko 18.

Katika mashindano hayo daraja la kwanza waliocheza mizunguko 18 kila mmoja, mchezaji Raju Lodhia alifanikiwa kutwaa nafasi ya kwanza kwa kupiga mikwaju 68 akifuatiwa na Tony Frisby kwa kupiga mikwaju 69.

Daraja la pili ya mizunguko 18 Monu Singh alishinda nafasi ya kwanza kwa kupiga mikwaju 66, akifuatiwa na Jatin Sonecha kwa kupiga mikwaju 70, huku daraja la tatu George Ogutu akishinda nafasi ya kwanza kwa kupiga mikwaju 73 akifuatiwa na  Jamal Mukarram aliyepiga mikwaju 74.

Aidha Abid Ogutu alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa wale waliozunguka mizunguko tisa kwa kupiga mikwaju 33 akifuatiwa kwa karibu na Murad Jivani aliyepiga mikwaju 34 huku  Jagdish Chuchu akitwaa ushindi kwa upande wa wazee.

Akizungumzia mashindano hayo kaptein wa timu ya Gymkana Robby Chadha alisema kuwa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya Gupta kwa miezi sita kuanzia January hadi june yana lengo la kuboresha club ya Gymkana kwa kufanya mashindano hayo kila wiki ya mwisho wa mwezi ambazo washindi watakuwa wanazawadiwa vikombe mbalimbali kutoka katika kampuni hiyo.


Kwa upande wa mshindi wa jumla, Monu Singh alisema kuwa mbali na kujiunga na club ya mchezo wa gofu kwa miezi sita pekee lakini amefanikiwa kutwaa ubingwa wa jumla kutokana na kucheza mchezo wa Hocky unaofanana na gofu kwa miaka 10 akiwakilisha timu ya Taifa ya Tanzania ambapo pia amekuwa akifanya mazoezi mara kwa mara kama sehemu ya mazoezi yake.

Mwisho……………………



0 comments:

Post a Comment