.

.
Wednesday, February 25, 2015

SHIRIKA la Mpango wa Chakula Duniani(WFP), limeanza kutoa mafunzo kwa
maafisa ugani katika mikoa ya Manyara na Arusha kukabili mabadiliko ya
tabia ya nchi yanayosababisha athari kubwa ya kukumbwa na ukame kwa
wakulima na wafugaji.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku tano jijini
hapa, afisa mwandamizi wa WFP,Juvenali Kisanga ,alisema mafunzo hayo
yatawapatia mbinu mbadala  ya kupangilia kilimo chao hasa katika
maeneo yaliyoathiriwa na ukame.
Alisema kwa mujibu wa tarifa zilizotolewa na wataalamu wa hali ya hewa
hapa nchini, zinadai kuwa huenda mwaka huu kukawa na uhaba wa
mvua,hivyo aliongeza kuwa hatua ya kutoa mafunzo hayo itasaidai kwa
maafisa ugani kutoa elimu kwa wakulima waweze kukabiliana na hali
hiyo.
Alisema mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni wa
miaka mitatu na kwamba nchi mbili za Malawi na Tanzania duniani
ziliteuliwa kwa majaribio.
''Huu mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni mpango
wa miaka mitatu ambao umeanza tangu mwaka jana na utaendelea hadi
2016,na unalenga kufanya majaribio kwa wakulima na wafugaji katika
maeneo yenye ukame.
Kwa upande wake afisa kilimo umwagiliaji na ushirika wilaya ya
Longido,Edward Kasiga alisema mafunzo hayo ni jitihada za kuondoa
changamoto ya ukame iliyopo katika wilaya ya Longido.
Aliongeza kuwa  katika kipindi cha nyuma wananchi waliathirika kwa
idadi kubw aya mifugo yao  kufa kwa njaa ,na rais Kikwete alisaidia
kugawa mifugo kwa wafugaji na chakula zaidi ya tani 3500 kwa wananchi
hao.
Alisema kwa kupitia maafisa ugani elimu ya kukabiliana na mabadiliko
ya nchi itawafikia wakulima na wafugaji na lengo ni kusambaza elimu
hiyo kwa wakulima wote katika maeneo ya majaribio

0 comments:

Post a Comment