.

.
Wednesday, February 25, 2015

Wadau wa soka la wanawake mkoani Arusha waiomba shirikisho la soka nchini TFF kuwasaidia kufanikisha uchaguzi wa chama hicho ambao umekuwa ukisua sua zaidi ya miaka 10 hali ambayo  inadidimiza kiwango cha mchezo huo mkoani hapa.

Aidha wenye dhamana ya kuhakikisha uchaguzi huo unakamilika mkoani ni chama cha soka mkoani Arusha ARFA umekuwa ukipiga danadana uchaguzi huo tangu mwaka juzi huku mashindano ya kitaifa ya wanawake yakifanyika chini ya ARFA ikiwemo fedha kwaajili ya mashindano hayo.

Kwa upande wake kaimu katibu wa chama hicho Pili Bonye alisema soka la wanawake Arusha linazidi kudumaa tofauti na mwanzo ilivyoanzishwa na hii inatokana na kutokuwa na uongozi halali kwani wao wanaokaim hawana sauti ya maamuzi juu ya utendaji wa maendeleo ya chama.

“Kutokana na tunaona hakuna mikakati yoyote ya kufanya uchaguzi kwa hapa Arusha tunaomba shirikisho la soka nchini kutusaidia kufanikisha hilo kwani tunaumia sana tunaposhindwa kufanikisha baadhi ya mikakati ya kuimarisha soka ka wanawake wakati kuna timu nyingi sana Arusha zaidi ya 10”

Soka hilo la wanawake linaloongozwa na Samweli Mpenzu (ambae ni mwanaume), pili alisema kuwa si haki chama hicho kiongozwe na wanaume wakati wanawake wapo hali ambayo inasababisha migongano kipindi cha mashindano kutokana na kukosekana maandalizi na kupelekea mwisho wa siku kubatiza moja ya tim za taasisi kuwa kama timu ya mkoa.

“huwezi amini mashindano yote tunayofanyaga ambayo wanawake wanahusishwa huwa tunachukua timu ya Testmony wakati ilitakiwa tuchague wachezaji wazuri kutoka timu mbali mbali katika wilaya zetu lakini hilo halifanyiki kwani hatuna hata chama cha mkoa licha ya wilayani na sisi tunaokaim hatuna sauti za utekelezaji ndio maana hata mashindano mengi tuko kama wasindikizaji tu hatufaidi zawadi”

Alisema kuwa anaishangaa TFF wanawake taifa kwa kutokujali ushiriki wa Arusha katika mikutano mikuu ya kitaifa, kwani wamekuwa na vikao na uchaguzi lakini wahana wawakilishi hivyo sasa wanataka kuwa miongoni mwa wajumbe, na kuwataka wasikilize kilio chao na mwezi march mwaka huu uchaguzi ufanyike.

Kwa upande wake kocha wa timu ya wanawake Arusha Geofrey Mrope alisema kuwa chama hicho kutokuwa na uongozi kunazidi kudidimiza soka la wanawake mkoani hapa hasa kutokana na kukosekana kwa mikakati ya kuliboresha

“Unajua hapa Arusha nimefundisha timu nyingi za wanawake na kuna vipaji vingi sana vya mpira tatizo hakuna uhamasishaji wala mikakati ya kuendeleza ikiwemo maandalizi ya kushiriki katika michuano mbalimbali huwa hakuna maandalizi na viongozi waliopo ukiwauliza hawana majibu ya moja moja nah ii imepelekea hata taifa cup tuishie mzunguko wa pili.”

Kwa upande wake katibu wa soka mkoa wa Arusha ambae ndie mwenye dhamana ya kuhakikisha chama hicho kinakuwepo alisema kuwa wanashindwa kufanya uchaguzi kutokana na kukosekana kwa wanawake wenye muamko na mchezo huo.

Mwisho……

0 comments:

Post a Comment