.

.
Tuesday, February 3, 2015

3:10 AM
Arusha. Kamanda wa polisi wilaya ya Arusha mjini (OCD) Mulilo Mulilo Amevitaka vikundi vya ulinzi shirikishi kuepuka kutumia dhamana hiyo kama sehem ya kuwanyanyasa wananchi na kuwaibia mali zao badala yake wawalinde kama ilivyo lengo la vikundi hivyo.

Kamanda Mulilo aliyasema hayo mapema jana alipokuwa akizindua vikundi viwili vya ulinzi shirikishi vilivyoko katika mtaa wa lolovono na Unga limited jijini Arusha vilivyojitolea kuunga mkono jitihada za jeshi la polisi kuwalinda wananchi wa maeneo hayo usiku na mchana sambamba na kutoa taarifa za matukia makubwa ya uhalifu katika mitaa yao.

Alisema kuwa mara nyingi wanavikundi wanaojitolea kufanya kazi ya ulinzi shirikishi wamekuwa wakijichulia sheria mkononi za kuwapiga wananchi huku baadhi yao wakitumia nafasi hiyo kama sehem ya kujipatia fedha kwa kuwatisha wahalifu ili wasiwachukulie hatua za kuwashitaki.

“Hivyo ndugu zangu nawaomba kikundi hiki kiwe cha kulinda wananchi na mali zao na pia muwe mnawashirikisha mambo mbali mbali ambayo mnafanya ikiwezekana mtunge sheria ndogo ndogo na mwenyekiti wenu na wananchi wote katika mikutano ya namna ya kuwaadhibu watu wa makosa madogo madogo sio kila kosa liletwe kituoni wakati linaweza kutatuliwa hukuhuku makwenu”

Mbali na hilo aliwataka kuwa na vitambulisho pamoja na mavazi sare (uniform) ambayo vitakuwa vinawatambulisha usiku na mchana sambamba na kuwa na mkakati kazi unaotambuliwa ili kuwafanya kujulikana utaratibu wa kazi zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo wa Lolovono Priscus Kwai alishukuru kuzinduliwa kwa kikundi hicho huku akiliomba jeshi la polisi kuangalia utaratibu wa kuwajengea kituo cha polisi katika eneo hilo kutokana na umbali wa kituo wanachokitegemea cha Unga limited huku wahalifu wengi wakizidi katika maeneo hayo hasa wanaofanya biashara za madawa ya kulevya, mirungi na watumiaji wa bangi pia.

Mwisho…………


0 comments:

Post a Comment