.

.
Wednesday, February 11, 2015

2:37 AM
na Bertha Ismail - Arusha

Wachezaji wa Timu za Arusha fc na Maafande wa Jkt Oljoro za mkoani hapa wameungana na timu zingine na kunufaika na elim ya sayansi ya soka sambamba na stadi pia mbinu za kucheza mpira bora lengo ikiwa ni kuifanya Arusha kupata timu tishio katika mechi za ligi mbalimbali watakazokutana nazo.

Wachezaji hao zaidi ya 60 walionufaika ni kutoka katika timu mbali mbali ikiwemo Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza pamoja na Arusha FC inayoshiriki ligi daraja la pli waliungana na timu zingine za Chacky FA,  Usa star na meru Worrious zinazoshiriki ligi daraja la tatu.

Mradi huo unaoratibiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru ilihusisha mafunzo ya siku 12 iliyotolewa katika kambi ya chuo cha maendeleo ya kimataifa kilichoko Arumeru mkoani Arusha na kutolewa na wakufunzi watatu akiwemo mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munassa Sabi pamoja na Kocha wa oljoro M’bwana Makata.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa kambi ya mafunzo hayo, mkuu wa wilaya Munasa Sabi alisema kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo baada ya kuona wachezaji wa timu mbali mbali za Tanzania wakicheza hovyo kwa kutumia nguvu zaidi kuliko Akili hali iliyopelekewa na nchi yetu kukosa shule ya soka kama nchi zingine.

“Unajua nchi za wenzetu kuna shule za soka ambazo watoto wenye vipaji vya soka walipelekwa shule maalum ya kuendeleza vipaji vyao  na baadae kutisha katika soka ndio maana unaona nchi za wenzetu watoto wa miaka kuanzia 15 wanacheza ligi kuu tofauti na sisi mtu mzima kabisa asie na mda mrefu uliobaki ndio anacheza ndio maana mimi nikaamua kuratibu mafunzo haya amabyo yatakuwa endelevu”

“Lengo kubwa ni kuzifanya kwanza timu za Arusha zikawe na makali ya aina yake kwenye timu watakazochezea hali itakayopandisha thamani zao na kucheza soka safi la kulipwa na kuwa kama ajira zingine zinazosomewa hivyo na soka lazima usome ili kujua mbinu na stadi za kucheza na kubuni nafasi ya kushinda”alisema mkuu huyo.

Mkuu huyo wa wilaya ambae alifanikiwa kuwapeleka vijana 10 nchini Brazil mwaka jana kushuhudia michuano ya kombe la dunia, alisema kuwa lengo kubwa ni kuwafanya vijana kuiga mbinu za soka la kimataifa ambapo mwaka huu ameahidi kuwapeleka vijana wengine zaidi ya 20 mwaka huu huko Europe.

“Unajua pamoja na kambi hii ambayo vijana wamepata semina ya sayansi na stadi za michezo kwa nadharia na vitendo lakini pia wanatakiwa washuhudie mechi mbali mbali na mazoezi ya timu za kimataifa ili kupata mbinu za wenzetu wanaofanikiwa kisoka hivyo lazima nijitahidi na wadau kuwafadhili waweze kuhudhuria michuano hiyo ili kufanikisha ndoto yetu ya kucheza kombe la dunia 2025”

Mwisho…………..

0 comments:

Post a Comment