.

.
Tuesday, February 3, 2015

kikosi cha timu ya Oljoro
Bertha Ismail 

Arusha - Timu ya maafande wa Jkt Oljoro yenye makazi yake jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja la kwanza kundi B’ msimu huu, imelaani vikali vitendo vinavyofanywa na shirikisho la soka nchini TFF juu ya kuwapeleka wachezaji wake muhimu katika mahakama ya michezo kwa kosa la kusingiziwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mwenyekiti wa timu hiyo Amosi Mwita alisema kuwa wameshangazwa na hali ya TFF kuwaita wachezaji wake tegemezi wa kikosi cha kwanza mbele ya kamati ya nidhamu kwa madai ya kufanya vurugu kwenye mechi kati yao na Bukinafo mjini morogoro.

“Jamani kwa kifupi tumepokea barua kutoka TFF za wito wa kuwaita wachezaji wetu wanne ambao ni Mlinda mlango tegemezi kwetu Dihe Makonga, Swalehe Hussein, Ramadhani Mwinyimbegu na Shaibu Nayopa kwenye kikao cha kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo february 3 mwaka huu kujitetea kwa madai kuwa  wameonekana wakifanya vurugu kwenye mechi Morogoro”

“Awali katibu wa kamati ya nidhamu inayoongozwa na Mwesigwa Selestine walilalamika kuwa wachezaji wetu hao walivamia benchi la wapinzani wetu Burkina faso sambamba na kumpiga refa Omary Matemela na kumchania nguo refa Klina Kabala Octoba 25, 2014 kwenye mechi tuliyocheza na burkinafaso kwenye uwanja Jamhuri ulioko Morogoro wakati baadhi ya wachezaji hao hata hawakuwa uwanjani na golikipa wetu alikuwa zake golini sasa iweje akampige mwamuzi? Tff ifikirie kwa undani kutusaidia hili”

“Hii tunaona kama tunafanyiwa hujuma kutokana na imeonekana tunashinda kwenda ligi kuu hivyo wapinzani wetu wanaamua kutumia kila njia kutudhoofisha kurudi nyuma, lakini naomba niseme tu kuwa jumatatu ya February 2 tutatua Dar na kesho yake jumanne tutaenda kwenye kikao hicho na tunaamini tutashinda kesi hii na kama kuna watu wanadhani hatupandi kwenda ligi kuu kwa fitina hizi wamechemsha kikubwa TFF watende tu haki”

Timu ya Oljoro iliyoko nafasi ya tatu kwa sasa Kundi B, inayoongozwa na Mwadui ya Sinyanga na Toto Afrika ya Mwanza, wamebakiza mechi mbili kumaliza  msimu wao wa ligi daraja la kwanza wakimalizia Tabora kwa timu ya Ryno na Polisi.

Aidha pamoja na kubakiza mechi cheche zaidi lakini wamekumbwa na balaa la wachezaji wake tegemezi kupuputika ikiwemo kuwakosa wachezaji wake wanne tegemezi waliokwenda kwenye mafunzo ya kijeshi hivi karibuni huku wengine wanne akiwemo mlinda mlango namba moja  wakikumbwa na kashfa hii ya kufanya fujo ambapo kama wakikutwa na makosa hayo watafungiwa kucheza mechi sita zilizoko mbele yao na kulipa faini ya 300,000 kila mmoja.

Mwisho………….

0 comments:

Post a Comment