.

.
Tuesday, July 28, 2015


 
MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA

Halmashauri ya jiji la Arusha limefanikiwa kuitimisha zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura kwa kuandikisha jumla ya wananchi 321,575, huku mkurugunzi wa jiji hilo akiwataka wote waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura.

Akizungumza na gazeti hili wakala wa uandikishaji jiji la Arusha, Iddi Juma ambaye pia ni Mkurugenzi wa jiji alisema kuwa awali walitarajia kuandikisha watu 265,087 lakini wamefanikiwa kuvuka lengo kwa zaidi ya asilimia 21 kwani wameandikisha watu 321,575 ambayo ni sawa na asilimia 121.

“Tunajivunia kuvuka lengo letu la idadi ya walioandikishwa lakini hatuwezi kujivunia kwa uandikishaji tu bali tutajivuania zaidi pale idadi hii waliyojiandikishwa wakijitokeza wote kupiga kura octoba kwenye uchaguzi mkuu wa kupata viongozi mbali mbali wa nchi”

“Nimesema hivyo kwa sababu vijana wengi walioonekana kupata vitambulisho hivyo walifurahia tu kuwa itawasaidia katika mambo yao binafsi lakini siyo kupia kura, lakini naomba niwaambie kuwa kupata kitambulisho ni jambo moja lakini kupiga kura ni jambo la msingi zaidi hasa ikizingatiwa ni haki ya msingi kupata kiongozi aliyepatikana kwa kura yako hivyo wajitokeze kwa wingi kupiga kura”

Mkuu huyo amesema kuwa kumekuwa na mazoea ya wananchi kutokujitokeza katika zoezi la upigaji kura kutokana na kuendekeza starehe pamoja na biashara na kusema kuwa swala hil ni kosa kwa sheria ya nchi hasa kutokana na gharama kubwa serikali inayotumia kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa hivyo kwa mwaka huu Arusha wasifanye kosa hilo bali wajitokeze kuchagua kiongozi wanaemtaka kwa maendeleo ya jiji, mkoa na nchi kwa ujumla.

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura jiji la Arusha lilianza june 16 na kufikia tamati julai 18 huku wanawake 160, 143 wakijiandikisha na wanaume 161, 432 katika vituo 183 katika kata 25 za jiji la Arusha.

“Katika zoezi hili naamini hakuna mtu asiyejiandikisha hasa baada ya kuruhusu watu wenye kazi au biashara wajiandikishe kwenye vituo vya biashara zao kutokana na ugumu wa kutoka, na pia hili linajidhihirisha siku tatu za mwisho hakukuwa na foleni kabisa kwenye vituo vya uandikishaji huku vituo vingine wakala wakikosa kabisa wateja la kushinda wakipiga soga hii inaonyesha kabisa watu wamemalizika na kama kuna watu wasiojiandikisha basi hawakutaka tu”

Mwisho…………

0 comments:

Post a Comment