.

.
Tuesday, July 28, 2015

7:32 AM
Bertha Ismail - Arusha

“Nimefurahi sana kuona  jinsi kiwango changu kinapanda na naamini hii ni mwanzo wa kutimiza ndoto zangu za kuwa mtaalamu wa mchezo wa gofu niweze kushindana kwa kulipwa na kuwa mchezaji maarufu wa mchezo huu na kuiwakilisha nchi yangu vema”.


Ni maneno ya kijana mdogo aliyeko kundi la Junior Mohamed Ally alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika michuano ya Arusha Open yaliyoshirikisha wachezaji 82 wa gofu kutoka mikoa mbali mbali nchini pamoja na nchi za Dubai na Kenya.

“Mimi ndoto zangu ni kuwa profesheno wa gofu nchini ili niweze kuwa mchezaji wa kulipwa na kuchuana katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kuitangaza nchi yangu hivyo watu wasishangae uwezo wangu wakalinganisha na umri wangu wa chini ya miaka 18 bali waangalie kipaji change na ndoto zangu ambazo siri hii ni mazoezi ya mara kwa mara kama sala kwangu”

Ally wa Arusha ametwaa ushindi wa jumla baada ya kupata nyavu 131,  (131 nett) katika kumbi 36 (36 halls) kwa siku mbili, huku kwa daraja la kwanza Richard Gomes (Arusha) akitwaa ushindi kwa kupata nyavu 152 nett akifuatiwa na Victor Joseph wa  Dar –es-salaam kwa kupata pia nyavu 152.

Kwa upande wa daraja la pili Prabvir Singh alitwaa ushindi kwa nyavu 146 akifuatiwa na Muzzafer Yusufally  kwa nyavu 156 wote wa Arusha na daraja la tatu Hiten Nathwan ambae ni mwenyekiti wa Arusha Gymkana Club kwa nyavu 150 akifuatiwa na Mona Singh kwa vyavy 151.

Akizungumzia mashindano hayo mwenyekiti wa mashindano kutoka chama cha Gofu Taifa alisema mashindano hayo ya Taifa yaliyoko kwenye kalenda ya TGU yana lengo la kutambua wachezaji wazuri wa machezo huo, kukuza vipaji vya vijana wadogo sambamba na kuvinoa vilivyopo.

“Kwanza niseme tu nimefurahishwa na uwezo mkubwa aliyoonyesha kijana mdogo Ally ukilinganisha na umri wake hali ambayo inatia moyo kuwa kwa sasa vilabu vina wachezaji wazuri watakaounda timu ya nchi yetu na kuna baadhi ya wachezaji wengine tumewaona na tutawaangalia tena kwenye michuano ya Taifa yatakayofanyika Moro goro”

“Lengo la mashindano hayo ya Morogoro ni kutafuta wachezaji wazuri watakaounda timu ya Taifa itakayokaa kambini kwa kujinoa kushiriki michuano ya nchi za  Afrika mashariki na kati yatakayofanyika Octoba nchini Kenya”

Mashindano hayo ya Arusha Open yaliyodhaminiwa na I&M bank yajulikanayo kama “I&M Golf Arusha Open” yameshirikisha wachezaji 82 kutoka vilabu vya Arusha, Dar, Moshi, TPC, Lugalo, Nairobi na Dubai.

Mwisho…………….

0 comments:

Post a Comment