Kamati
ya Utendaji ya Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF iliyokutana
jumapili Februari 22 mwaka huu, imefanya mabadiliko ya mahali
utakaofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka Mkoa wa Sinigida na
kuhamishia mkoa wa Morogoro.
Hatua hiyo
imefikiwa na Kamati ya Utendaji kutokana na sababu za kutokukamilika kwa
miundombinu ya mkutano mkuu na kuwepo ka shughuli nyingine za kijamii
mkoani humo.
Kamati ya Utendaji inamshukuru Mwenyekiti wa Chama
cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida (SIREFA), na uongozi mzima kwa
kujitolea kuandaa mkutano huo na huko nyuma waliweza kuandaa mkutano wa
makatibu wa vyama vya soka vya mikoa.
TFF itaandaa vikao na
matukio mengine mkoani Singida itakapotokea hapo baadae, tarehe ya
mkutano mkuu itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14, 15 mwaka huu
Home
»
»Unlabelled
» badala ya Singida, TFF yahamishia mkutano Morogoro
Wednesday, February 25, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment