jiji la Arusha kutumia bilioni 42 mwaka 2014/ 2015 7:37 AM Bertha Mollel Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha vijijini ,Fidelis Lumato amesemakuwa wilaya yake imepanga bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 42 kwa mwaka wa fedha 2015 /2016 ambazo zitaelekezwa kwenye masuala ya maji,afya na elimu ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii. Fidelis Lumato aliyasema hayo jana katika kikao cha Halmashauri hiyo kilichojadili bajeti hiyo jana ambapo amefafanua kuwa mambo hayo matatu ni vipaumbele muhimu kwa halmashauri hiyo.Amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha maabara,mabweni pamoja na kujenga vituo vya afya karibu. Lumato amesema kuwa upatikanaji wa fedha hizo utasaidia ujenzi wa barabara ya Redio Habari Maalumu,Ngaramtoni,Seliani na Sambasha ambazo pia ni ahadi za Raisi Jakaya Mrisho kikwete. Naye Mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye amesema kuwa ni vyema halmashauri ikajikita zaidi kuboresha shule za msingi na sekondari ikiwemo shule ya Sekondari Sokon 2 ambayo inakabiliwana uhaba wa matundu ya choo. Medeye amewataka wananchi na madiwani kuwa wavumilivu baada ya mashimo ya nguzo kuchimbwa kwenye maeneo yao bila kuwekewa umeme kwanimradi wa umeme vijijini (REA) bado uko kwenye utekelezaji hadi utakapofikia kikomo juni 30 mwaka huu. “Nawaomba madiwani na wananchi muwe wavumilivu badonafuatilia juu ya mradi wa REA bado wanaendelea na utekelezaji kwasasa kasi yaoinaenda kadiri wanavyopata fedha serikalini” Alisema Medeye Diwani wa Kata ya Mwandeti Boniface Tarakwa amesemakuwa bajeti hiyo ilenge kukarabati barabara ambazohazipitiki hasa kipindi cha mvua ili kuboresha miundombinu .
0 comments:
Post a Comment