Wadau wa
soka la wanawake mkoani Arusha waiomba shirikisho la soka nchini TFF kuwasaidia
kufanikisha uchaguzi wa chama hicho ambao umekuwa ukisua sua zaidi ya miaka 10
hali ambayo inadidimiza kiwango cha
mchezo huo mkoani hapa.
Aidha wenye
dhamana ya kuhakikisha uchaguzi huo unakamilika mkoani ni chama cha soka mkoani
Arusha ARFA umekuwa ukipiga danadana uchaguzi huo tangu mwaka juzi huku
mashindano ya kitaifa ya wanawake yakifanyika chini ya ARFA ikiwemo fedha
kwaajili ya mashindano hayo.
Kwa upande
wake kaimu katibu wa chama hicho Pili Bonye alisema soka la wanawake Arusha
linazidi kudumaa tofauti na mwanzo ilivyoanzishwa na hii inatokana na kutokuwa
na uongozi halali kwani wao wanaokaim hawana sauti ya maamuzi juu ya utendaji
wa maendeleo ya chama.
“Kutokana na
tunaona hakuna mikakati yoyote ya kufanya uchaguzi kwa hapa Arusha tunaomba
shirikisho la soka nchini kutusaidia kufanikisha hilo kwani tunaumia sana
tunaposhindwa kufanikisha baadhi ya mikakati ya kuimarisha soka ka wanawake
wakati kuna timu nyingi sana Arusha zaidi ya 10”
Soka hilo la
wanawake linaloongozwa na Samweli Mpenzu (ambae ni mwanaume), pili alisema kuwa
si haki chama hicho kiongozwe na wanaume wakati wanawake wapo hali ambayo
inasababisha migongano kipindi cha mashindano kutokana na kukosekana maandalizi
na kupelekea mwisho wa siku kubatiza moja ya tim za taasisi kuwa kama timu ya
mkoa.
“huwezi
amini mashindano yote tunayofanyaga ambayo wanawake wanahusishwa huwa
tunachukua timu ya Testmony wakati ilitakiwa tuchague wachezaji wazuri kutoka
timu mbali mbali katika wilaya zetu lakini hilo halifanyiki kwani hatuna hata
chama cha mkoa licha ya wilayani na sisi tunaokaim hatuna sauti za utekelezaji
ndio maana hata mashindano mengi tuko kama wasindikizaji tu hatufaidi zawadi”
Alisema kuwa
anaishangaa TFF wanawake taifa kwa kutokujali ushiriki wa Arusha katika
mikutano mikuu ya kitaifa, kwani wamekuwa na vikao na uchaguzi lakini wahana
wawakilishi hivyo sasa wanataka kuwa miongoni mwa wajumbe, na kuwataka
wasikilize kilio chao na mwezi march mwaka huu uchaguzi ufanyike.
Kwa upande
wake kocha wa timu ya wanawake Arusha Geofrey Mrope alisema kuwa chama hicho
kutokuwa na uongozi kunazidi kudidimiza soka la wanawake mkoani hapa hasa
kutokana na kukosekana kwa mikakati ya kuliboresha
“Unajua hapa
Arusha nimefundisha timu nyingi za wanawake na kuna vipaji vingi sana vya mpira
tatizo hakuna uhamasishaji wala mikakati ya kuendeleza ikiwemo maandalizi ya
kushiriki katika michuano mbalimbali huwa hakuna maandalizi na viongozi waliopo
ukiwauliza hawana majibu ya moja moja nah ii imepelekea hata taifa cup tuishie
mzunguko wa pili.”
Kwa upande
wake katibu wa soka mkoa wa Arusha ambae ndie mwenye dhamana ya kuhakikisha
chama hicho kinakuwepo alisema kuwa wanashindwa kufanya uchaguzi kutokana na
kukosekana kwa wanawake wenye muamko na mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment