Arusha - Timu ya
maafande wa Jkt Oljoro yenye makazi yake jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja
la kwanza kundi B’ msimu huu, imelaani vikali vitendo vinavyofanywa na
shirikisho la soka nchini TFF juu ya kuwapeleka wachezaji wake muhimu katika
mahakama ya michezo kwa kosa la kusingiziwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa, Mwenyekiti wa timu hiyo Amosi Mwita alisema
kuwa wameshangazwa na hali ya TFF kuwaita wachezaji wake tegemezi wa kikosi cha
kwanza mbele ya kamati ya nidhamu kwa madai ya kufanya vurugu kwenye mechi kati
yao na Bukinafo mjini morogoro.
“Jamani kwa
kifupi tumepokea barua kutoka TFF za wito wa kuwaita wachezaji wetu wanne ambao
ni Mlinda mlango tegemezi kwetu Dihe Makonga, Swalehe Hussein, Ramadhani
Mwinyimbegu na Shaibu Nayopa kwenye kikao cha kamati ya nidhamu ya shirikisho
hilo february 3 mwaka huu kujitetea kwa madai kuwa wameonekana wakifanya vurugu kwenye mechi
Morogoro”
“Awali katibu
wa kamati ya nidhamu inayoongozwa na Mwesigwa Selestine walilalamika kuwa
wachezaji wetu hao walivamia benchi la wapinzani wetu Burkina faso sambamba na
kumpiga refa Omary Matemela na kumchania nguo refa Klina Kabala Octoba 25, 2014
kwenye mechi tuliyocheza na burkinafaso kwenye uwanja Jamhuri ulioko Morogoro
wakati baadhi ya wachezaji hao hata hawakuwa uwanjani na golikipa wetu alikuwa
zake golini sasa iweje akampige mwamuzi? Tff ifikirie kwa undani kutusaidia
hili”
“Hii tunaona
kama tunafanyiwa hujuma kutokana na imeonekana tunashinda kwenda ligi kuu hivyo
wapinzani wetu wanaamua kutumia kila njia kutudhoofisha kurudi nyuma, lakini
naomba niseme tu kuwa jumatatu ya February 2 tutatua Dar na kesho yake jumanne
tutaenda kwenye kikao hicho na tunaamini tutashinda kesi hii na kama kuna watu
wanadhani hatupandi kwenda ligi kuu kwa fitina hizi wamechemsha kikubwa TFF
watende tu haki”
Timu ya
Oljoro iliyoko nafasi ya tatu kwa sasa Kundi B, inayoongozwa na Mwadui ya
Sinyanga na Toto Afrika ya Mwanza, wamebakiza mechi mbili kumaliza msimu wao wa ligi daraja la kwanza wakimalizia
Tabora kwa timu ya Ryno na Polisi.
Aidha pamoja
na kubakiza mechi cheche zaidi lakini wamekumbwa na balaa la wachezaji wake
tegemezi kupuputika ikiwemo kuwakosa wachezaji wake wanne tegemezi waliokwenda
kwenye mafunzo ya kijeshi hivi karibuni huku wengine wanne akiwemo mlinda
mlango namba moja wakikumbwa na kashfa hii
ya kufanya fujo ambapo kama wakikutwa na makosa hayo watafungiwa kucheza mechi
sita zilizoko mbele yao na kulipa faini ya 300,000 kila mmoja.
Mwisho………….
0 comments:
Post a Comment