na Bertha Ismail - Arusha
Wachezaji wa
Timu za Arusha fc na Maafande wa Jkt Oljoro za mkoani hapa wameungana na timu
zingine na kunufaika na elim ya sayansi ya soka sambamba na stadi pia mbinu za
kucheza mpira bora lengo ikiwa ni kuifanya Arusha kupata timu tishio katika
mechi za ligi mbalimbali watakazokutana nazo.
Wachezaji
hao zaidi ya 60 walionufaika ni kutoka katika timu mbali mbali ikiwemo Oljoro
inayoshiriki ligi daraja la kwanza pamoja na Arusha FC inayoshiriki ligi daraja
la pli waliungana na timu zingine za Chacky FA,
Usa star na meru Worrious zinazoshiriki ligi daraja la tatu.
Mradi huo
unaoratibiwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru ilihusisha mafunzo ya siku 12
iliyotolewa katika kambi ya chuo cha maendeleo ya kimataifa kilichoko Arumeru
mkoani Arusha na kutolewa na wakufunzi watatu akiwemo mkuu wa wilaya ya Arumeru
Nyirembe Munassa Sabi pamoja na Kocha wa oljoro M’bwana Makata.
Akizungumza
baada ya kumalizika kwa kambi ya mafunzo hayo, mkuu wa wilaya Munasa Sabi
alisema kuwa wameamua kufanya mafunzo hayo baada ya kuona wachezaji wa timu
mbali mbali za Tanzania wakicheza hovyo kwa kutumia nguvu zaidi kuliko Akili
hali iliyopelekewa na nchi yetu kukosa shule ya soka kama nchi zingine.
“Unajua nchi
za wenzetu kuna shule za soka ambazo watoto wenye vipaji vya soka walipelekwa
shule maalum ya kuendeleza vipaji vyao
na baadae kutisha katika soka ndio maana unaona nchi za wenzetu watoto
wa miaka kuanzia 15 wanacheza ligi kuu tofauti na sisi mtu mzima kabisa asie na
mda mrefu uliobaki ndio anacheza ndio maana mimi nikaamua kuratibu mafunzo haya
amabyo yatakuwa endelevu”
“Lengo kubwa
ni kuzifanya kwanza timu za Arusha zikawe na makali ya aina yake kwenye timu
watakazochezea hali itakayopandisha thamani zao na kucheza soka safi la kulipwa
na kuwa kama ajira zingine zinazosomewa hivyo na soka lazima usome ili kujua
mbinu na stadi za kucheza na kubuni nafasi ya kushinda”alisema mkuu huyo.
Mkuu huyo wa
wilaya ambae alifanikiwa kuwapeleka vijana 10 nchini Brazil mwaka jana
kushuhudia michuano ya kombe la dunia, alisema kuwa lengo kubwa ni kuwafanya
vijana kuiga mbinu za soka la kimataifa ambapo mwaka huu ameahidi kuwapeleka
vijana wengine zaidi ya 20 mwaka huu huko Europe.
“Unajua
pamoja na kambi hii ambayo vijana wamepata semina ya sayansi na stadi za
michezo kwa nadharia na vitendo lakini pia wanatakiwa washuhudie mechi mbali
mbali na mazoezi ya timu za kimataifa ili kupata mbinu za wenzetu wanaofanikiwa
kisoka hivyo lazima nijitahidi na wadau kuwafadhili waweze kuhudhuria michuano
hiyo ili kufanikisha ndoto yetu ya kucheza kombe la dunia 2025”
Mwisho…………..
0 comments:
Post a Comment