Arusha. Kamanda wa
polisi wilaya ya Arusha mjini (OCD) Mulilo Mulilo Amevitaka vikundi vya ulinzi
shirikishi kuepuka kutumia dhamana hiyo kama sehem ya kuwanyanyasa wananchi na
kuwaibia mali zao badala yake wawalinde kama ilivyo lengo la vikundi hivyo.
Kamanda
Mulilo aliyasema hayo mapema jana alipokuwa akizindua vikundi viwili vya ulinzi
shirikishi vilivyoko katika mtaa wa lolovono na Unga limited jijini Arusha
vilivyojitolea kuunga mkono jitihada za jeshi la polisi kuwalinda wananchi wa
maeneo hayo usiku na mchana sambamba na kutoa taarifa za matukia makubwa ya
uhalifu katika mitaa yao.
Alisema kuwa
mara nyingi wanavikundi wanaojitolea kufanya kazi ya ulinzi shirikishi wamekuwa
wakijichulia sheria mkononi za kuwapiga wananchi huku baadhi yao wakitumia
nafasi hiyo kama sehem ya kujipatia fedha kwa kuwatisha wahalifu ili
wasiwachukulie hatua za kuwashitaki.
“Hivyo ndugu
zangu nawaomba kikundi hiki kiwe cha kulinda wananchi na mali zao na pia muwe
mnawashirikisha mambo mbali mbali ambayo mnafanya ikiwezekana mtunge sheria
ndogo ndogo na mwenyekiti wenu na wananchi wote katika mikutano ya namna ya
kuwaadhibu watu wa makosa madogo madogo sio kila kosa liletwe kituoni wakati
linaweza kutatuliwa hukuhuku makwenu”
Mbali na
hilo aliwataka kuwa na vitambulisho pamoja na mavazi sare (uniform) ambayo
vitakuwa vinawatambulisha usiku na mchana sambamba na kuwa na mkakati kazi
unaotambuliwa ili kuwafanya kujulikana utaratibu wa kazi zao.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa mtaa huo wa Lolovono Priscus Kwai alishukuru kuzinduliwa kwa
kikundi hicho huku akiliomba jeshi la polisi kuangalia utaratibu wa kuwajengea
kituo cha polisi katika eneo hilo kutokana na umbali wa kituo wanachokitegemea
cha Unga limited huku wahalifu wengi wakizidi katika maeneo hayo hasa
wanaofanya biashara za madawa ya kulevya, mirungi na watumiaji wa bangi pia.
Mwisho…………
0 comments:
Post a Comment