Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya
kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari
wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki
iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.
Bodi
inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu
na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko
salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.
Aidha
Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni mwisho wa
kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo
vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na
masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo
kupita.
Bodi
inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na
masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha
wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia
anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
0 comments:
Post a Comment