.

.
Sunday, August 25, 2013

3:47 AM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimck5I-_vQ4Lwe-pCXpvt3KHwU-ccLuOgWZGn4bD_8sJRH3NF-J49iKOIa0Dufe2lWPu62SxJlgxtMgbZHgYQCF74pTVBuTxZhz-FlplzhXPfYL0nMKUS7q4ca70H8zEumnsMbAFl7MLK1/s1600/Lyumba.jpg 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni imetupilia mbali pingamizi la mke wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba, Aurelia Ngowi la kupinga mumewe kuuza mali za familia na kumfukuza kwenye nyumba wanayoishi.

Kesi hiyo imefunguliwa mbele ya Hakimu Jackline Rugemalila katika mahakama hiyo, Dar es Salaam. Mahakama hiyo ilihamia Mbezi Africana iliko nyumba hiyo kufan

ya ukaguzi ili kujiridhisha juu ya pingamizi zilizotolewa na pande zote mbili.
 
Ngowi alipinga mumewe kuuza mali za familia na kumfukuza, wakati kesi ya msingi ya madai ya talaka ikiendelea, jambo ambalo Liyumba akiongozwa na Wakili wake, Sweetbert Nkuba alikuwa akilipinga, kwa kudai nyumba hiyo ni ya biashara na si ya kuishi familia, kama inavyodaiwa.

 
“Baada ya kusikiliza pande zote mbili, mahakama hii imeona kuwa nyumba hiyo ni ya biashara na si ya kuishi familia, kama ilivyoelezwa katika zuio la mshitaki,” alisema Hakimu Rugemalila.

 
Katika hati ya madai, Aurelia anaiomba mahakama iweke zuio la muda ili Liyumba asiuze mali za familia, pia asiuze nyumba iliyopo Africana Mbezi Beach katika kiwanja namba 2232/2233, ambayo walikuwa wanaitumia kama makazi ya familia.

 
Anaiomba mahakama iamuru waendelee kuishi katika nyumba hiyo, wakati shauri hilo la likiendelea, pia alipe gharama za uendeshaji wa kesi.


Katika hati ya kiapo, inayounga mkono madai yake, Aurelia anadai alifunga ndoa na Liyumba mwaka 1978 mkoani Kilimanjaro na kupata watoto wanne.

 
Anadai mwaka 1980 walianza kuishi kwenye nyumba iliyopo Africana. Anadai waliendelea kuishi katika nyumba hiyo na baadaye waliamua upande wa nyumba, waweke hoteli inayoitwa Amjen Executive pamoja na biashara nyingine, zilizokuwa zinawaingizia kipato kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya familia.

 
Kwa mujibu wa hati ya kiapo, baada ya Liyumba kutoka gerezani ambako alikuwa anatumikia kifungo, alihama nyumbani na kuanza kuuza mali mbalimbali yakiwemo magari, kiwanja cha ekari 50 kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani na kiwanja cha Tabata.

 
Alidai kuwa Julai 18 mwaka huu, Liyumba aliwafukuza yeye na watoto wake na kufunga nyumba hiyo pamoja na eneo la biashara, waliyokuwa wakiitegemea kwa ajili ya kupata fedha za matumizi ya kila siku, kisha akaweka walinzi ambao wanawazuia kuingia.

 
Aurelia alidai baada ya kufanya uchunguzi, aligundua kuwa mume wake anauza mali walizochuma pamoja. Alidai endapo mahakama haitaweka zuio, atapata hasara kubwa. Liyumba alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma.

 
Alimaliza kutumikia kifungo hicho Septemba 23 mwaka juzi. Kesi ya msingi ya madai ya talaka, itatajwa tena Septemba 16, mwaka huu.
chanzo jumamtanda blog.
 

0 comments:

Post a Comment