.

.
Wednesday, October 2, 2013


 

Mke wa Sheikhe Ponda Issa Ponda, Khadija Ahmad kushoto akimpungia mkono mumewe Ponda Issa Ponda mara baada ya Ponda kusikiliza kesi inayomk
abili katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro jana.
Sheikhe Ponda akitelemka katika basi maalum lililomleta kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro jana.
Sheikhe Ponda Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi mkali mara baada ya kutemka katika basi lililomleta katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kusikiliza kesi inayomkabili mkoani Morogoro ambapo kesi hiyo itasikiliza tena Nov 7 mwaka huu.
Wakili wa muda wa Sheikhe Ponda Issa Ponda, Yahaya Njawa akizungumza jambo na Sheikhe Ponda muda mfupi kabla ya kupandishwa kizimbani.
Njawa kulia akizungumza jambo na Sheikhe Ponda baada ya kesi yake kughailishwa katika mahakama hiyo jana.
 
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa wamekunja ngumi huku wakitamka maneno ya kiaraba "Taqri allah Akiball yakiwa na maana ya mungu mkubwa" wakati wakielekea katika msikiti mkuu wa mkoa wa Morogoro kupata maelezo ya Sheikhe Ponda kutokana na baadhi yao kushindwa kusikiliza kesi hiyo, hapa ni barabara ya zaamani ya Dar es Salaam eneo la Lotto wakitokea mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.
Mke wa Sheikhe Ponda Issa Ponda, Khadija Ahmad kulia akiwa amejumuika na waumini wa dini ya kiislam kwenda katika msikiti mkuu wa mkoa wa Morogoro kupata maelezo juu ya kesi inayomkabili mumewe katika barabara ya zamani ya Dar es Salaam kufuatia baadhi ya waumini hao kushindwa kusikiliza kesi kutokana na uwingi wao katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.
Askari magereza kikosi maalum akipita mbele ya askari wenzake wakati akielekea eneo la mahakama ili kuimarisha ulinzi wakati wa kesi hiyo.
Ulinzi ulikuwa mkali sana, hapa askari kanzu akitumia kifaa maalum chenye uwezo wa kupaini chuma kilichopo katika begi ama mfuko katika nguo.

Ombi la kufutiwa shitaka moja liliwakilishwa na Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro, mahakamani hapo Septemba 17, mwaka huu, akitaka shitaka la kwanza la kutotii amri halali linalomkabili mteja wake lifutwe. 

Wakili Nassoro alidai kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria kusikiliza shitaka hilo, vinginevyo lifunguliwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Kesi hiyo imeahiriswa mpaka Novemba 7 mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza mashahidi wa kesi hiyo. Sheikh Ponda amerudiswa rumande.

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro leo imetupilia mbali ombi la kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda. 

Ponda anakabiliwa na mashitaka matatu; ambayo ni kutokutii amri halali, kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa. 
chanzo:jumamtanda
 

0 comments:

Post a Comment