.

.
Tuesday, October 29, 2013

2:27 PM

Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
Sehemu za mwili alizojeruhiwa na baba yake.

Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.


KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.

Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.

Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.

Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kisha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.

Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.

Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa ndani ya jamii.

Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.

Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.

Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.
CREDIT: MBEYA YETU

0 comments:

Post a Comment