Mkutano
wa siku mbili wa kamati ya
Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa kwamba Ziwa Manyara lipo
hatari ya
kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uharibifu wa
mazingira kunakotokana na kilimo pembezoni mwa mito kama juhudi za
maksudi hazikuchulia kutunza mazingira yanayozunguka maeneo ya mito
mbalimbali inayoingia ziwani humo.
Hali jii imetokana na kuongezeka kwa shughuliza kibianadamu hussani za kiuchumi na kusababisha pia ziwa
manyara kujaa udongo na matope pamoja uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akiwasilisha mada kuhusu changamoto za uhifadhi katika hifadhi ya ziwa
Manyara,Muikolojia katika hifadhi hiyo Bibi
Christina Kiwanga amesema kukosana
kwa utashi wa kisiasa ni changamoto kubwa katika kuliokoa ziwa hilo.
Bibi Kiwanga ametaja changamoto
nyingine ni pamoja na kukosekana kwa mipango endelevu katika baadhi ya vijiji kuhusu
umuhimu wa uhifadhi sanjari na elimu.
Muikolojia huyo amewambia wajumbe wa kamati ya Ushauri
ya Mkoa wa Arusha kwamba shughuli za Biandamu hususani za kilimo na za
kiuchumi zimechangia kwa kiwango kikubwa
hifadhi hiyo kuwa katika hatari ya kutoweka.
Naye Meneja Ujirani Mwema makao makuu
ya Tanapa BWANA Ahmed Mbugi amesema
umuhimu wa maeneo ya Mapito ya (SHOROBA) na mitawanyiko ya wanyama
katika hifadhi amesema asilimia 80 ya Shooba
zilizokuwepo miaka ya nyuma zimetoweka kabisa.
Amesisitiza kwamba ni lazima wananchi
walinde uasilia wa mapito ya
wanyama pori kutokana na umuhimu wa maeneo hayo
Mbungi amefafanua kwamba awali
kulikuwa na Maeneo ya SHOROBA yenye
ukubwa wa ekari 40,000 katika hifadhi za
Arusha Kilimanjaro,manyara lakii maeeo haya yamepungua.
Aidha amesisitiza kwamba wanasiasa wanachangia
kuhujumu maeneo haya ya uhifadhi
kutokana na kukosekana kwa kuchukuwa maamuzi
mazito ya kuyalinda maeneo hayo kwa kuogopa wapiga kura hali inayoleta
changamoto mbalimbali pindi wanapotoa taarifa za kulinda maeneo hayo.
Pia ameeleza kwamba asilimia 70 ya
mapato yanayotokna na uhifadhi
yanatumika katika usajidia utekelezaji w amiradi ya kijamii ikiwemo ya afya,elimu,
maji, na miradi ya barabara.
Amesema migongano baina ya
wanyamapori na binadamu inachangiwa na
binadamu kuingilia maeneo ya mapito ya wanyamapori hivyo kuwakosesha njia za kupita hali inayoharibu mazingira.
Amesisitiza kwamba hatua hii inasababisha kuathiri shughuli za
utalii ambapo idadi ya watalii hupungua sanjari na shughuli za uchumi kuathirika
Mbali na hali hii katika kipindi cha mwaka 1957/63 na 1987/`988 uoto
wa asilimia hususani misitu ulipungua kwa asilimia 13.5
wakati maeneo ya kilimo
yaliongezeka kwa asilimia 10.9.
Aidha
maeneo ya ushorobo yaliyotumika kwa
shughuli za kilimo kati ya mwaka 1997/98 yaliongezeka kati ya asilimia 8.35 hadi 11.41
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Karatu Lazaro Maasae yeye amesema kasi ya ziwa manyara kuendeleoa kujaa ugondo na
matope ni ya kasi zaidi
0 comments:
Post a Comment