NA mwandishi wetu,
Maiti ya
mwanamke Emeliana Kibuga(42) mkazi wa kijiji cha Kash Babati vijijini anaedaiwa
kuuawa na askari wa hifadhi ya Tarangire octoba 16 inaendelea kusota katika
chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Babati.
Hali hii
imaetokana na ndugu kususia mwili huo kwa madai kuwa polisi wanawakinga wauaji
wa ndugu yao huku wakishindwa kutoa taarifa sahihi juu ya mauaji hayo ambapo
wamedai kuwa hawatauzika mwili huo ambapo kama hawatapokea taarifa hiyo basi
wataupeleka mwili huo kwa mkuu wa mkoa ukakae hapo hadi kupata taarifa za
mauaji ya ndugu yao.
Kwa mujibu
wa ndugu wa marehem ambae ni mwenyekiti wa mtaa wa Unjej bwana Rashid Kijogoo
alisema kuwa mume wa marehem alitekwa na askari wa hifadhi hiyo ya Tarangire octaba
14 saa nane za usiku nyumbani kwake kijijini hapo Kash na kumwacha mkewe lakini
pia octaba 16 mkewe ambae kwa sasa ni
marehem nae alitekwa na askari hao hao na kupelekwa kusikojulikana.
Alisema kuwa
askari hao 6 wakiwemo wanawake wawili walifika katika kitongoji hicho na
kumchukua marehem nyumbani kwake majira ya saa nne asubuhi kwa madai ya kwenda
kufanya mahojiano nae na kumrudisha majira ya jioni huku akiwa chini ya ulinzi
mkali wa askari hao wakiwa na silaha za
moto ambapo pia mwanamke huyo alionekana akivuja dam sehemu mbalimba;li za
mwili wake.
Alisema kuwa
baaada ya kufika nyumbani hapo askari hao walionekana kumhoji jambo marehem na
kuondoka nae kwa mara nyingine ambapo kwa mara hii marehem hakuonekana tena
hadi octoba 17 mwili wake ulipookotwa katika pori la hifadhi ya Tarangire huku
akiwa amengolewa meno, na kutobolewa macho pamoja na kuvunjwa shingo.
Kijogoo
alisema kuwa mwili huo unaodaiwa kuokotwa na askari wa hifadhi ya Tarangire
ulipelekwa katika hospitali ya Wilaya, Mrara.
Kwa upande
wake mtoto wa marehem aliyejulikana kama Christina Elias Kibuga alisema kuwa
octoba 16 majira ya saa kumi jioni walikuja Watu sita wakiwemo wanawawe wawili
waliovalia kiraia na wanaume wane, mmoja akiwa amevalia sare za jeshi la
wananchi Tanzania (JWZT) ambapo walikuja na mama yao huku wakimhoji kwa ukali,
“Ilikuwa ni
saa kumi jioni ikiwa ni siku mbili tangu baba atekwe usiku na siku hiyo nae
mama alitekwa asubuhi na kurudishwa jioni na askari hao sita, mmoja akivalia
nguo za jeshi walimleta mama yetu huku akiwa anavuja dam sehem nyingi na
kumgombeza kuwa wawaonyeshe kitu alichosema kiko nyumbani, mama yetu alinyamaza
tu ndipo walipomwambia tena kuwa kumbe hutaki bali umetusumbua bure kuja hadi
huku, sasa leo utatutambua, wakaondoka nae tena hadi leo hatujamuona tena bali
tunasikia kuwa ameuawa” alisema mtoto huyo huku akibubujikwa na machozi
mfululizo.
Kwa upande
wake kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Akili mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio
hilo la mauaji, alikiri kuuawa kwa mwanamke huyo na kukanushwa kuuawa na askari
hao kwa madai kuwa mwanamke huyo alikufa kwa mshutuko wa kuhojiwa.
Hata hivyo
jambo hili limepingwa vikali na ndugu pamoja na majirani wa marehem huyo kwa
madai kuwa mwili huo ulikutwa ukiwa na majereha mwili mzima iikiwemo kutobolewa
macho, kuvunjwa shingo na meno kuonyesha kipigo kikali juu ya ndugu yao pia
sehem za siri kuchubuka ambayo ni dhahiri ndugu yao alibakwa.
Nae Daktari
wa hospitali ya wilaya ya Babati, Dr. Palagyo alithibitisha marehemu huyo
kutobolewa macho, kuvunjwa shingo pamoja na meno sambamba na kuvuja dam sehem
za siri hali iliyopelekea kifo chake.
Utekaji huo
uliosababisha mauaji ya mwanamke huyo unafuatiwa na operesheni maalum ya kusaka
majangili wanaojihusisha na uwindaji haramu wa meno ya tembo katika hifadhi
mbalimbali za Taifa unaoendelea hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment