WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta,
amesema Tanzania itatoa talaka kwa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda
ambazo zimeamua kuanzisha Jumuiya ya hiari nje ya Jumuiya ya Afrik
a
Mashariki.
Sitta alisema kutokana na nchi hizo kuonekana kuitenga Tanzania na
Burundi ambazo ni wanachama wa jumuiya hiyo, wameshaanza mazungumzo ya
kushirikiana kiuchumi, kisiasa na nchi za Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC).
Kauli hiyo ya Sitta inatokana na mikutano ya mara kwa mara
inayofanywa na marais Uhuru Kenyata wa Kenya, Paul Kagame (Rwanda) na
Yoweri Museveni (Uganda) kuzungumzia masuala mbalimbali ya kushirikiana
nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Waziri Sitta alibainisha msimamo wa Tanzania kutengwa na nchi hizo
tatu jana bungeni, alipokuwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali
waliokuwa wakitaka kujua kauli ya serikali juu ya vikao vinavyofanywa na
marais hao watatu.
Mbunge wa Viti Maalumu Rukia Ahmed (CCM), aliitaka serikali ipeleke
pendekezo bungeni la kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla
haijapewa talaka kutoka kwa Rwanda, Uganda na Kenya ambazo zimekuwa
zikifanya mikutano inayojadili masuala ya jumuiya bila kuihusisha
serikali ya Tanzania.
Akijibu hoja hiyo Sitta, alisema ni mapema kwa Tanzania kupeleka
bungeni hoja ya kujitoa katika jumuiya hiyo kwa kuwa kinachofanywa na
nchi hizo kimeshafikishwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi
wanachama ambaye atakitolea ufafanuzi katika kikao kitakachofanyika
wiki mbili zijazo.
Sitta alifafanua kauli ya Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, hivi karibuni ya kwamba
Tanzania inasubiri talaka akisema yenyewe ndiyo yenye uwezo wa kutoa
talaka kwa jumuiya hiyo kwa kuwa inamiliki asilimia 52 ya eneo lote
huku nchi zilizobakia zikigawana asilimia 48 iliyobakia.
“Hawa wenzetu wanafanya utoto wa kutuzunguka, sisi tunatumia hekima
za mzee Mwinyi aliyesema ‘mwongo, mwongoze’. Kama wao wana hila zozote
juu yetu, siku si nyingi tutazibaini, kama ni ndoa kwenye jumuiya basi
sisi ndio tutakuwa tumeoa…hivyo tutatoa talaka wakati wowote,” alisema.
Naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), aliitaka
serikali isiendelee na hatua zozote kwenye jumuiya hiyo ambayo
inaonekana kuelekea kuvunjika.
Akijibu swali hilo, Sitta alisema serikali haijakaa kimya bali
imeamua kutoshiriki vikao vyote ambavyo nchi za Kenya, Rwanda na Uganda
zitakuwa zimeshayazungumzia masuala husika na kuamua kuwa na msimamo wa
pamoja nje ya jumuiya.
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alihoji serikali inangoja
utafiti gani juu ya kutengwa kwao kiuchumi na nchi hizo tatu wakati
Kenya wameshaingia makubaliano ya kibiashara na Ethiopia na Sudan.
Katika jibu lake, Sitta alisema Tanzania imeshafanya mazungumzo na
nchi za DRC na Burundi kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
Alisema kuwa DRC ndiyo yenye manufaa makubwa kiuchumi kwa Tanzania
kuliko Rwanda, Uganda, Kenya na Burundi kwa sababu mizigo mingi
hutegemea bandari ya Dar es Salaam.
“Burundi nao wanatengwa kama tunavyofanyiwa sisi, lakini tumeamua
kushirikiana kikamilifu na DRC pamoja na Burundi ambao tuna imani wana
manufaa makubwa kwetu,” alisema.
Hivi karibuni Tanzania iliingia kwenye mgogoro na Rwanda baada ya
Rais Jakaya Kikwete kutoa ushauri kwa Rais wa Rwanda, Kagame kuketi
chini na waasi wa nchi hiyo ili kuzungumzia masuala ya amani kwa nchi
yao. TANZANIA DAIMA
Home
»
»Unlabelled
» TANZANIA KUTOA TARAKA KWA NCHI ZA RWANDA, KENYA NA UGANDA.
Thursday, October 31, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment