.

.
Saturday, January 4, 2014

12:23 AM
Wakazi wa eneo hilo wakiangalia eneo la ajali.



Watu wawili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ngema katika eneo la Mlima Terati lililopo halmashauri ya jiji la Arusha wakati wakiwa wanapakia moramu kwenye gari aina ya Isuzu lori  jana saa 3:30 asubuhi.

 Mmoja wa marehemu hao ametambulika kwa jina la Joseph Solomoni huku mwingine bado hajafamika mara moja.

Janga hili lililofungua mwaka 2014 ni janga lililotokea ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu kufariki dunia kwa watu 13 katika machimbo ya Moram yaliyoko Moshono jijini hapa ambapo viongozi mbalimbali wa mkoa na sekta ya madini walitoa amri kufungwa kwa machimbo yote yasiyokuwa na kibali wala kufuata sheria za machimbo.

Tukio hilo lililoshtua wengi limezua minong'ono kuwa "Je tamko la viongozi hao ilikuwa zuga ya huzuni ya ndugu wa marehem waliouawa kipindi hicho....au ilikuwa siasa za kujitafutia umaarufu??

Tukio hilo lililokuwa kama janga la kitaifa si la mkoa pekee kila kiongozi wakiwemo hata viongozi wa dola waliahidi kulifuatilia matamko mbalimbali yaliyotolewa na viongozi kwa kukagua machimbo yote huku naibu Waziri wa madini Masele akiahidi pia kulivalia njuga machimbo hayo yasiue tena, lakini matokeo yake leo tunasikia ndugu zetu tena wameuawa kwa kuangukiwa na ngema.

 hivi jamani utendaji wa viongozi wetu wa kuwatumikia wananchi na kuwalinda ni nguvu ya soda pindi tu inapofunguliwa gesi hutoka kwa kasi na kutulia baada ya mda mfupi ndivyo na utendaji ulivyo kuwa unashughulikiwa kwa maneno pale janga linapotokea lakini vitenda ni adim??

nisiseme sana nikanukuliwa kwa haya ila kila mtu atafakari matamko ya viongozi wetu wanayoyatoa kwenye majanga na matukio mbalimbali yanayogharim maisha ya watanzania wenzetu.

Nanyi viongozi tafakarini matamko mnayoyataka kuyatoa kama mtaweza kutekeleza kabla ya kutamka na baadae kuishia mitini kwani mnatuweka katika chuki na kisasi watanzania mnaotuwakilisha.
                               
huzuni ilivyotawala eneo la tukio.


0 comments:

Post a Comment