.

.
Saturday, January 4, 2014

9:58 AM
picture of elephant 
DAR ES SALAAM. 
KAMA Tembo wa Tanzania wangeulizwa kuna jambo gani kubwa hawatalisahau kwa mwaka 2013, bila shaka jibu lingekuwa: “Tuliwindwa, tukauawa sisi na watoto wetu na bado tuna hofu.”


Ingawa tembo ni mnyama mbabe awapo porini, lakini uwezo wake wa kujilinda yeye na jamii yake ulipunguzwa nguvu kwa kiwango kikubwa mwaka 2013, baada ya mauaji ya hazina hiyo ya taifa kuongezeka kwa kiasi kikubwa hata kuisukuma Serikali kuanzisha Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kila mwezi tembo 850 wanauwawa. 
Utekelezaji wa operesheni hiyo ambao ulilenga kuzuia uwindaji haramu wa wanyama hao na wengine walio katika mbuga na hifadhi za taifa huku taarifa zikionyesha kuwa shehena kubwa ya pembe za ndovu ambayo imekuwa ikikamatwa ndani na nje ya nchi. 


Ripoti ya operesheni hiyo, ilileta athari kubwa kwa wananchi na mifugo hatua iliyomlazimu Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wanne waliokuwa wakiisimamia wizara zilizotajwa kuzembea katika kusimamia Opereesheni Tokomeza Ujangili.

Mawaziri hao ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

Hata hivyo, akizungumza katika salamu zake za Mwaka Mpya, Rais Kikwete alisema: “Tunakamilisha matayarisho ya kuanza awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza. Ni muhimu kuendelea nayo kwani tusipofanya hivyo majangili wataendelea na vitendo vyao viovu.

Kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili nchini, Mkataba wa Biashara ya Kimataifa kwa Viumbe vilivyo Hatarini (CITES), uliitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi nane duniani zinazoongoza kwa kufanya biashara ya pembe za ndovu.

Matukio yaliyotikisa
Polisi mjini Zanzibar hawataisahau Novemba 15, 2013, siku waliyopigwa na butwaa baada ya kukamata shehena kubwa ya pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi, zikiwa na thamani ya Sh7.4 bilioni.

Awali mzigo huo ulikuwa umehifadhiwa katika Mtaa wa Darajabovu, mkoa wa Mjini Magharibi, kabla ya kusafirishwa hadi Malindi.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kuwa baada ya kukamilika kwa kazi ya kupakua na kuhesabu pembe hizo, walibaini kuwa vilikuwa vipande 1,021 vikiwa na uzito wa kilo 2,915.

Tukio jingine la kufunga mwaka ni lile lililotokea jijini Dar es Salaam, ambalo lilisimamiwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Tarish Maimuna ambapo pembe za ndovu 706 zilikamatwa.

Katika tukio hilo, ambalo lilithibitisha kuuawa kwa tembo 353, raia watatu wa China wakazi wa Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, walikutwa wakiwa wamehifadhi shehena hiyo nyumbani kwao. 


Watuhumiwa hao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung.                                                                                            MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment