.

.
Sunday, January 12, 2014


Fortunatha Ringo.
 
MWANDISHI wa Kujitegemea aliyekuwa akiandikia gazeti la HabariLeo kutokea Manyara Fortunatha Ringo ambaye alifariki dunia juzi anatarajiwa kuagwa leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Ubungo Kibangu.Kanisa hilo lipo mbele ya Stendi ya daladala ya Makoka mbele kidogo ya Kituo cha Riverside.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu shughuli ya kumuaga mwandishi huyo inatarajiwa kuanza saa sita na baada ya ibada mwili utasafirishwa kwa maziko Kilimanjaro.

Maziko hayo yanatarajiwa kufanyika Jumatatu.

Habari kutoka kwenye familia yake, zinasema kwamba mwandishi huyo ambaye alizaliwa Dar es Salaam Septemba 25, 1980 alifariki akisubiri tiketi ya kwenda India kwa matibabu.

Dada wa mwandishi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Glad alisema kwamba ndugu yake alikuwa na matatizo ambayo kitaalamu yanaitwa SLE na alikuwa anakwenda India kwa matibabu.

Inaaminika matatizo hayo yalitokana na athari za dawa ya malaria aliyoitumia ambayo ilikuwa na salpha mwaka 2011.

Alisema alishatibiwa Muhimbili na alipangiwa matibabu zaidi nchini India.

0 comments:

Post a Comment