.

.
Friday, January 31, 2014

7:10 AM
Makazi ya muda ya waathirika wa mafuriko kijiji cha Mateteni baada ya nyumba zao kumoka kutokana na maji ya mafuriko hayo. PHOTO/MTANDA BLOG



MOROGORO. 

KAMATI ya Maafa Mkoa wa Morogoro inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Kilosa, Elias Tarimo imeshindwa kutoa takwimu za waathirika wa mafuriko ndani ya siku moja kama ilivyoagizwa na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki iliyopita.



Mafuriko hayo yalitokea katikati ya wiki iliyopita Kijiji cha Magole na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu. Pia, yalisomba nyumba, vyakula na vifaa mbalimbali vya nyumbani, mahakama na shule.


Akizungumza na Redio One jana, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alisema kazi inaendelea kwa sababu wanataka kuhakiki watu halisi waliopatwa na maafa hayo.


“Tunataka kutumia fursa hii kumwambia Rais kuwa tulighafilika hata kutoa takwimu zile za watu 12,000, ambazo (Rais) alisema hazina uhalisia... kwa sasa tunataka kufanya uhakiki wa kina tujue thamani ya hasara,” alisema Bendera na kuongeza:


“Tunataka kujua hasa mali zilizoharibiwa, kuna nyumba zilizobomoka kabisa, kuna zilizoingiliwa na maji lakini hazikubomoka, kuna zilizoharibiwa nusu, kuna watu wangapi wanahitaji misaada ya haraka na huduma nyingine.”


Mwandishi wa habari hizi aliyefika eneo la tukio, alishuhudia kazi ya uhakiki ikiendelea maeneo yaliyoathirika huku Tarimo akishiriki kufanya kazi hiyo.


“Kazi ipo hatua za mwisho hadi leo (jana) jioni tunatarajia kukamilisha uhakiki na kumkabidhi mkuu wa mkoa...kwa sasa tupo hatua za mwisho mwisho na itakapokuwa tayari nitawapatia bila kuficha,’’ alisema Tarimo.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alisema wilaya inaendelea na uhakiki na kwamba, watatoa taarifa baada ya kukamilika ambayo itakuwa

0 comments:

Post a Comment