.

.
Tuesday, January 7, 2014

10:38 AM
                                            JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                                             WIZARA YA MAMBO YA NDANI
                                                 JESHI LA POLISI TANZANIA

                                                                                                          

                          TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUTOKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
TAARIFA YA AJALI ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU SABA
MNAMO TAREHE 04/01/2014 MUDA WA 4:15 USIKU MAENEO YA MTI MMOJA WILAYANI MONDULI BARABARA YA ARUSHA - DODOMA, GARI AINA YA MITSUBISHI FUSSO LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 795 CMC LILILOKUWA LINAENDESHWA NA ALEX S/O KESSY MKAZI WA NGARAMTONI LILIGONGANA NA GARI AINA YA SCANIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 495 ASW LILILOKUWA LINAENDESHWA NA DEREVA ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA ALFAYO MKAZI WA KIMANDOLU.
AJALI HIYO ILITOKEA WAKATI GARI AINA YA SCANIA LIKIWA LINATOKEA ARUSHA KUELEKEA MAKUYUNI NA MITSUBISHI FUSO LILIKUWA LINATOKEA MAKUYUNI KUELEKEA NGARAMTONI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU SABA AMBAO NI:-
PETRO S/O HENRY MKAZI WA UNGA LTD, (2) ALFAYO DEREVA WA SCANIA, (3) MAMA PETER MKAZI WA OLDONYOSAMBU, (4) MAMA NORBERT MKAZI WA SAKINA, (5) DADALA D/O BOYA MKAZI WA OLDONYOSAMBU (6) ALEX KESSY MKAZI WA NGARAMTONI AMBAYE PIA NI DEREVA WA FUSSO NA WA MWISHO NI MAMA NTANGAI MKAZI WA OLDONYOSAMBU.
BADO JESHI LA POLISI MKOANI HAPA TUNAENDELEA KUFUATILIA MAJINA HALISI YA MAREHEMU. CHANZO CHA AJALI HIYO BADO HAKIJAFAHAMIKA NA MIILI YOTE YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI CHA HOSPITALI YA MOUNT MERU. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

 IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI,
(SACP) LIBERATUS SABAS       TAREHE 06/01/2014

0 comments:

Post a Comment