WILAYA ya Kiteto imeingia kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya kinyama baada ya wakulima kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kugombea ardhi.
Miongoni mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)
Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyinyizia nyumba zao mafuta aina ya petrol kisha kuwasha moto
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani.
“Nilichomewa Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo vyakula, lakini nilichonusuri ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huo.
Hata hivyo baada ya kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa kulifika Kitongojini lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa madai kuwa ni uongo kwamba hakuna watu waliokusanyana
Akielezea hayo Mwenyekiti huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi kujiona kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi katika upande mmoja
Kwa upande wake Lairumbe Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya akizungumzia sakata hilo alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni muongo kwani baada ya wao kufika kabla ya tukio alikataa kuwataja wahusika
Hata hivyo kauli hiyo ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti huyo wa Kitongoji kuonyesha udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya kufika hawakuweza hata kukubali kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa kimasai
“Baada ya kufika walitaka nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka twende eneo la tukio wakakata nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha wakarejea Kiteto ambapo usiku vijana hao wakatekeleza azima yao ya kuchinja mtu mmoja na kumpiga mwingine risasi kisha kuwajeruhi watu saba”alisema Mwenyekiti huyo wa kitongoji
Waliofariki katika uvamizi huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo (33) ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo pamoja na watu wengine saba kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na mapanga
Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias (21) Juma Bahati (13) Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma Martin pamoja na Musa Juma (16) aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu
Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika kitongoji hicho aliwapa siku 30 viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kuwatambua wananchi hao ili kuondoa tofauti zao waweze kufanya kazi bila bughdha
“Ninyi wananchi mwende kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani maisha bora kwa wananchi yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa sasa hamna hata moja”alisema Mbwillo,
Chanzo, jumamtanda blog
0 comments:
Post a Comment