Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Dar es Salaam,Tanzania
Matumaini yalikuwa makubwa sana mwaka 1961 Taifa letu lilipojikomboa kutoka
makucha ya ukoloni. Vita 3 - Umasikini, Ujinga na Maradhi zilitangazwa. Azimio
la Arusha likawa tumaini kubwa la kutokomeza umasikini, hasa wa vijijini.
Ni kweli tumepiga hatua kwenye Nyanja kadhaa. Ni dhahiri kuwa kwenye maeneo
mengi tumerudi nyuma sana. Uwezo wetu wa kuzalisha Mali na kuondoa umasikini
umepungua ambapo sasa uchumi unakua kwa wastani wa asilimia 7 lakini umasikini
haupungui kwa sababu sekta ya wanyonge-kilimo,
imedumaa.
Takribani mazao yetu yote ya kilimo tunauza nje kama ghafi tofauti na
miaka ya 1970 ambapo tulianza kuongeza thamani kama Korosho, Kahawa, Pamba na
Katani. Tumerudishwa nyuma na ubinafsishaji na menejimenti za hovyo hovyo.
Elimu sasa ni bora elimu na sio elimu bora maana
watoto hawajifunzi mashuleni na hata wahitimu wa vyuo vikuu uwezo wao kukabili
changamoto za nchi makazini ni mdogo sana.
Afya ya wananchi bado mbaya
kutokana na wananchi wengi kufariki kwa magonjwa yanayotibika. Miaka 52
baada ya Uhuru ni asilimia 6 ya Watanzania wana hifadhi ya jamii.
Wakulima wetu
bado hawana bima ya mazao yao wala pensheni. Changamoto ya kizazi cha sasa
cha viongozi ni ku transform nchi ili kuongeza uwezo wa uzalishaji, kuongeza
ajira, kupunguza inequality na kujenga Taifa imara mbele ya mataifa.
Home
»
»Unlabelled
» ZITTO AWEKA WAZI MAPUNGUFU YA TANZANIA MIAKA 52 YA UHURU
Tuesday, December 10, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment