Mkazi wa Kijiji cha Mbugu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Anina Shaban (28) akiwa wodini.
INAWEZEKANA wapo wagonjwa wanaopelekwa chumba cha kuhifadhia maiti
(mochwari) wakiwa hai. Huenda wengine hufia humo baada ya kuzidiwa na
baridi la chumba hicho sambamba na kukosa hewa. Piga picha ni wewe !
Lakini kwa kijana Anina Shaban
(28) mkazi wa Kijiji cha Mbugu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, yeye
alibahatika, kwani aliishia kwenye lango la kuingia mochwari akidhaniwa
ameshakufa.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni akiwa
ndani ya wadi ya Sewa Haji kitengo cha MOI katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Dar alikolazwa kwa miezi 9 sasa, Anina anasema:
“Siwezi kuisahau siku ile, ninachoweza kusema kwa urahisi sana ni Mungu
tu ndiye aliyependa nisife kwa wakati asiokubaliana nao, vinginevyo leo
ningekuwa kaburini.
“Ilikuwa mwezi wa tatu, tarehe ishirini na nne nakumbuka, siku hiyo
nilitua hapa Dar kwa mara ya kwanza nikitokea kijijini kwetu.
“Lengo
la kuja Dar lilikuwa kutafuta maisha mazuri, maana vijana wenzangu
waliotangulia kuja kila waliporudi kusalimia waliniambia maisha bora
yapo kwenye Jiji la Dar es Salaam. Moja ya mguu uliovunjika.
“Niliamini kwani hata mavazi yao yalionesha kwamba kweli wana maisha
mazuri. Sasa ni nani asiyetaka maisha mazuri? Ndipo nikaamua kuja Dar
siku hiyo.
“Lakini ndoto
zangu ziligonga mwamba mara tu niliposhuka Kimara. Nilivuka barabara
kwenda upande wa pili nikiwa na begi langu lenye nguo mbili tatu, ghafla
daladala lilitokea na kunigonga, nikaanguka na kupoteza fahamu! Ilikuwa
ajali kubwa sana.
“Nilipopata fahamu nilijikuta nikiwa hapa Muhimbili, lakini nikiwa
katika hali isiyokuwa ya kwangu, mikono, miguu ilifungwafungwa. Nilianza
kulia huku nikiwa sijui hapa ni wapi.
“Daktari mmoja alipita na kuniona nikilia, akaja na kuniuliza
kilichoniliza, nikamjibu hali nilionayo, ndipo akanisimulia kwamba
nilipata ajali mbaya sana Kimara wakati nikivuka barabara.
“Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuuliza ajali hiyo ilitokea
lini, akaniambia mwezi mmoja uliopita. Ina maana mimi nilikuwa katika
hali ya kutojitambua kwa muda wote huo. Anina Shaban, ndani ya wodi ya Sewa Haji kitengo cha MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar.
“Cha ajabu, aliniambia nilifikishwa hapa si kama majeruhi bali kama maiti ya mtu aliyekufa kwa kugongwa na gari.
“Daktari
huyo alisema walionileta kila mmoja alijua nimeshaaga dunia kufuatia
ajali ile. Hivyo nilikuwa napelekwa moja kwa moja mochwari.
“Daktari aliendelea kunieleza kuwa hakuna aliyejua kwamba bado nilikuwa
hai kwani nilikuwa siangaliki kutokana na majeraha makubwa
niliyoyapata.
“Hata hivyo,
kabla sijaingizwa mochwari daktari mmoja alitaka kujiridhisha kwanza
kama kweli nilishafariki dunia, ndipo akagundua kuwa bado nilikuwa hai
kwani nilikuwa napumua kwa mbali sana.
“Nilikuwa nimeumia vibaya mno. Nilivunjika mikono yote, tena mara mbilimbili, nilivunjika miguu yote na mbavu tatu.
“Nilifikishwa
hospitalini nikiwa nimekunjwa kama mtu anavyobeba nyama kwenye mfuko wa
rambo. Mwacheni Mungu aitwe Mungu jamani, siamini kama kweli leo hii
naweza kukaa mwenyewe.
“Nilijiuliza nilipata wapi mkosi huo? Mbona niliwaaga vizuri tu wazazi
wangu kwamba nakuja Dar kutafuta ajira na walinikubalia kwa vile katika
watoto watatu katika familia yetu, mimi ndiyo mtoto wa kwanza na wote
tulikuwa nyumbani tukiendelea na kilimo cha jembe la mkono.
“Nilijua hapa Dar ningepata kibarua hata cha kuwakatia ng’ombe majani
au kuwasombea wajenzi matofali lakini kwa bahati mbaya sikuyafikisha
malengo niliyoyakusudia.
“Kinachoniuma na kunitoa machozi ni kuwaona wagonjwa wenzangu
wanatembelewa na ndugu zao, wanawafariji na kuwaletea vyakula lakini kwa
upande wangu hakuna hata mmoja.
“Kule kijijini wazazi hawana simu, mimi hapa pia sina simu, ni vigumu
kuwajulisha, nahisi wanaamini tayari nimeshapata kibarua lakini
siwakumbuki.
“Wangejua wangenifuata kunichukua na kunirudisha kijijini kwetu,” Anina alisema na kuanza kulia.
“Wagonjwa
tuliolazwa nao wengi wameshapona na kuruhusiwa kurejea makwao. Lakini
nasikitika kwamba nilitoka nyumbani mzima nitarudi na ulemavu,” akalia
tena.
“Nitakwenda kuwapa
wazazi wangu kazi ngumu ya kunitunza kama mtoto mdogo, hakuna jinsi
inabidi niyakubali matokeo, najua huu ndiyo mwisho wangu wa utafutaji,
nimebakia mtu wa kitandani, sikuyapenda maisha haya bali ndivyo Mungu
alivyonipangia natembea lakini si kama zamani,” alisema kijana huyo.
Aliwaomba Watanzania ambao wangependa kumsaidia watumie namba hii 0713 413098.
Naye
Afisa Mkuu Msaidizi Mambo ya Jamii Kitengo cha Mifupa MOI, Matua Frank
alisema Anina anaendelea vizuri na wakati wowote wanaweza kumsafirisha
kwenda kwenda kijijini kwao.
“Kwa sasa tunajiandaa kumsafirisha, tumempatia matibabu kwa kipindi
chote hicho kwa gharama ya hapa hospitali hadi sasa amepata nafuu kwa
kiasi
chanzo; jumamtanda
Home
»
»Unlabelled
» nusura kuingizwa mochwari kudhaniwa kufariki dunia.
Tuesday, December 10, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment