Kiongozi wa kwanza wa Kenya huru, Rais Jomo Kenyatta.
KENYA inayozingatiwa kuwa injini ya uchumi katika Afrika ya Mashariki
inaadhimisha miaka 50 ya uhurui katika muhtadha wa kesi inayomkabili
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake kwenye Mahakama ya mjini The Hague
ICC.
Tokea mwaka
wa 2010 Kenya inaongozwa katika msingi wa katiba mpya ya kidemokrasi.
Ustawi wa uchumi ni wa juu, unaovuka asilimia tano licha ya kasoro ya
ufisadi. Na kugunduliwa hivi karibuni kwa mafuta maana yake ni ustawi
zaidi kwa nchi hiyo.
Mapambano dhidi ya Al-Shabaab.
Kwa sasa majeshi ya Kenya yanashiriki katika juhudi za kuleta amani
nchini Somalia kama sehemu ya majeshi ya Umoja wa Afrika (AMISOM).
Kutokana na Kenya kushiriki katika juhudi hizo za kulinda amani nchini
Somalia, magaidi wenye itikadi kali ya kiislamu wa Al -Shabaab
wanalipiza kisasi kwa kufanya mashambulio ya kikatili mara kwa mara
nchini Kenya.
Taifa la vijana
Shujaa wa vita vya Mau Mau, Gitu wa Kahengeri.
Zaidi
ya asilimia 60 ya Wakenya ni watu wenye umri wa chini ya miaka 24.
Tulikutana na vijana wa Kenya katika mkahawa wa internet mmojawapo
katika jiji la Nairobi waliokuwa wanayatafakari maendeleo ya nchi yao
katika maadhimisho ya mwaka wa 50 wa uhuru wakiwa na wasi wasi lakini
pia wakiwa na matumaini na fahari juu ya yaliyofikiwa nchini mwao.
Wasemayo vijana juu ya uhuru
Sibyle Munika amesema idadi kubwa ya watu bado wanaishi katika
umasikini, hawana mahala pakuishi na wala hakuna nafasi za ajira za
kutosha kwa ajili ya vijana.Amesema anatamani kuwa na viongozi wazuri
wasiokuwa mafisadi.
Joane Ochieng Onyango anayesomea taaluma ya
vyombo vya habari ameeleza kuwa Kenya inasonga mbele katika tekinolojia
lakini bado pana changamoto kubwa,kwa sababu "nchi yetu bado
haijaendelea vizuri"
Na Samuel amejitambulisha kuwa
anashughulika na mambo ya ugavishaji.Yeye ametuambia kwamba hali ya
vijana wa leo ni nzuri kuliko ya wale wa miaka 50 iliyopita kwa sababu
ameeleza kuwa vijana wa leo wananufaika na tekinolojia ya kisasa na zana
za kileo za kupatia habari.
Ni kweli kwamba sekta ya
tekinolojia ya mawasiliano na habari inastawi nchini Kenya. Wakenya ni
wabunifu. Wanatayarisha programu za kompyuta kukidhi mahitaji ya
wakulima, kwa ajili ya kutoa habari juu ya mambo ya afya au
wanatayarisha programu za kuwezesha kufanya miamala ya fedha kwa njia ya
simu, maarufu kama MPesa.
Silicon Savannah
Victor Bwire wa Baraza la Vyombo vya Habari la Kenya.
Kiasi ya humusi moja ya pato jumla la ndani inahawilishwa kwa njia ya
simu ya mkononi. Karibuni tu Kenya itakuwa kituo kikuu cha tekinolojia -
Silicon Savannah ya Afrika,mithili ya Silicon Valley ya Carlifonia.
Wakati wa machafuko mnamo mwaka wa 2008 watayarishaji wa mipango ya
kompyuta wa Kenya, Ushahidi, walizindua jukwaa la mawasiliano ili kutoa
habari juu ya matukio ya umwagikaji damu katika sehemu za mizozo .Habari
hizo ziliwasilishwa kwa watu katika ujumbe wa simu za mkononi.Wakati
huo watu walihisi kwamba hawakupata habari za kutosha kutoka kwenye
vyombo vya habari vya kawaida.
Mswada wa kudhibiti maudhui ya habari
Kenya ina mawanda mapana katika mandhari ya vyombo vya habari.Lakini
wakati huo huo wabunge wamewasilisha kwa Rais Uhuru Kenyatta mswada wa
sheria wa kuipa serikali mamlaka makubwa ya kuyadhibiti maudhui ya
vyombo vya habari.
Victor Bwire ambae ni makamu mwenyekiti wa
baraza huru la vyombo vya habari nchini Kenya amekasirishwa na mswada
huo kwa sababu uhuru wa vyombo vya habari ni jambo lililowekwa katika
katiba ya Kenya.
Bwire amesema kwamba mswadaa huo una
vipengele vinavyokiuka katiba.Vipengele hivyo vinaigeuza kazi ya
waandishi kuwa ya kihalifu.
Rais Uhuru Kenyatta (kulia) na Rais Mstaafu Mwai Kibaki.
Hata
hivyo Rais Kenyatta bado hajautia saini mswada huo.Kwa sasa ametingwa
na kesi inayomkabili kwenye Mahakama Kuu ya Kimataifa ya mjini The
Hague.
Kwa kuvitumia vidokezo dhidi ya ubeberu, Kenyattta
anawahamasisha watu barani Afrika wasisimame dhidi ya Mahakama ya mjini
The Hague ICC na anajaribu kufanya juhudi ili kesi yake iahirishwe au
ikiwezekana aweze kuikwepa kabisa.
Rais Kenyatta pamoja na Makamu wake
William Ruto wanakabiliwa na mashtaka ya kutenda uhalifu dhidi ya
ubinadamu kuhusiana na matukio ya umwagikaji damu yaliyofuatia uchaguzi
wa mwaka wa wa 2007.
Mtanziko kwa nchi za magharibi
Nchi za Ulaya zinataka kesi hiyo ifanyike dhidi ya Kenyatta, lakini
wakati huo huo Kenya ni mshirika muhimu wa nchi za magharibi katika
harakati za kupambana na ugaidi.
Kenya inashiriki katika harakati hizo
nchini Somalia. Imeyapeleka majeshi yake yanayopigana kama sehemu ya
majeshi ya Umoja wa Afrika. DW Kiongozi wa kwanza wa Kenya huru, Rais Jomo Kenyatta.

majeshi ya Umoja wa Afrika. DW
Home
»
»Unlabelled
» MIAKA 50 YA UHURU KENYA.
Thursday, December 12, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment