-->
Wakati tunaelekea msimu huu wa sikuu ya Chrismass na mwaka
mpya, matukio ya kutisha ya ubakaji na mauaji ya watoto wachanga na kutupwa
katika maeneo mbali mbali yanazidi kukithiri mkoani Arusha.
Matukio hayo yaliyokwisha ripotiwa na BERTHA BLOG bado
yanaendelea kukithiri kwa kasi ya ajabu tena kwa idadi kubwa mkoani hapa huku
baadhi yake yakishuhudiwa na Blog hii na mengine yakitaarifiwa na wasamaria
wema na Jeshi la polisi lakini ni baadhi tu yaliyothibitishwa na jeshi hilo.
Baadhi yao ni matukio
mawili yaliyoripotiwa na Blog hii ya ubakaji ya
mtoto wa miaka miwili kubakwa na kijana wa miaka 20, sambamba na ubakaji
wa mtoto wa darasa la tatu kubakwa na mzee wa miaka 40 huku yote hayo
yakishindwa kuthibitishwa na jeshi la polisi.
Mbali na matukio hayo ya ubakaji pia jeshi la polisi mkoani
Arusha limeshindwa pia kuthibitisha taarifa za matukio ya unyama wa mauaji ya watoto wachanga
wanaozaliwa na kutupwa huku baadhi yao
wakitolewa kabla ya umri wa kuzaliwa (miezi 9).
Baadhi ya matukio ya watoto wachanga kuuawa na kutupwa ni
pamoja na lile lililotokea octoba 24 ambapo mtoto mchanga mwenye jinsia ya kike
mwenye umri wa siku moja alikutwa ametupwa kichakani chini yam lima kivesi akiwa ndani ya ndoo eneo la
kijenge juu kata ya kimandolu jijini Arusha.
Kitoto kichanga kilichookotwa kijenge juu kikiwatupwa kikiwa ndani ya ndoo |
Kwa mujibu wa mashuhuda na wajuzi wa mambo, walisema kuwa
mtoto huyo alikwisha fikia umri wa kuzaliwa ambapo kama
inavyoonekana inasadikiwa mtu huyo alikuja kujifungulia hapo na kumweka mtoto
huyo kwenye ndoo na kumwacha na yeye kutokomea pasipojulikana.
Aidha BERTHA BLOG ilishuhudia kichanga hicho majira ya saa 1
asubuhi ambapo jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kukichukua kichanga
hicho, na baadae majira ya saa tatu alikamatwa dada ambaye hakuweza kutambulika
jina lake kwa haraka kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo lakini hadi leo jeshi
la polisi halijaweza kuthibitisha kupokea taarifa ya kutokea kwa tukio hilo.
baadhi ya watu waliojitokeza kushangaa tukio hilo la mtoto huyo akiwa ndani ya ndoo |
Afisa
wa polisi akiuchukua mwili wa mtoto huyo uliofungwa na kanga
uliootolewa na msamaria mwema mda mfupi baada ya kutaarifiwa kuhusu
tukio hilo |
Tukio lingine la kuuawa na kutupwa kwa watoto wachanga
limetokea desemba 16 eneo la sekei wilaya ya Arumeru, ambapo mtoto mchanga
ambaye hakuweza kutambulika jinsia wala umri aliokotwa kwenye daraja pembezoni
mwa barabara ya lami ya kuelekea mahakamani baada ya wasamari wema kutoa
taarifa kwa jeshi la polisi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa mtoto huyo alikuwa kati ya
umri wa miezi 7 au 8 ambapo mtuhumiwa inaonekana na alitoa mimba hiyo kabla ya
kufikia miezi ya kujifungua.
Katika tukio lingine limetokea desemba 17 eneo la mzunguko
wa Njiro na kijenge, ambapo mtoto mchanga mwenye jinsia ya kiume alikutwa amekufa
na kutupwa kwenye mtaro uliopo pembezoni mwa barabara hiyo aliyesadikiwa kuwa
na umri wa miezi 6-8.
Aidha taarifa hiyo imethibitishwa jana na jeshi la polisi na
kusema kuwa mtoto huyo aliokotwa na jeshi la polisi majira ya saa tatu asubuhi
na mwili wake kufanyiwa uchunguzi na kuhifadhiwa katika hospitali ya moa Mount
meru huku upelezi ukiendelea wa kumpata muhusika wa tukio hilo .
Katika kutothibitisha matukio ya nyuma kwa madai kuwa
hayajamfikia bodo na upelelezi unaendelea wa kubaini matukiop hayo, kamanda wa
polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema “kiukweli matukio hayo ndio
kwanza unanieleza hivyo ngoja nitamuuliza OC-CID na akinipa taarifa hizo
nitawapa….. ila kama ni kweli nitoe tu wito
kwa watanzania kuwa waache kutupa watoto hovyo…”alisema kamanda Sabas na
kuongeza.
“Watambue kuwa hata watoto hao wana haki ya kuishi na kama hawawezi kulea kwa kuipata kwa bahati mbaya basi
wasiwatupa bali wawapeleke kwenye vituo na taasisi mbali mbali za kulele watoto
yatima kuliko kuwauwa watoto hao kwaajili ya sababu zao binafsi”.
0 comments:
Post a Comment