Rais wa Kenya , Mwai Kibaki amewaaga rasmi wakazi wa
Arusha na Watanzania wote kwa ujumla wakati akihitimisha kazi yake ya mwisho
mjini hapa akiwa kama mwenyekiti wa marais wa
jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kazi ya Mwisho
ya Rais Kibaki ilikuwa ni kulizindua jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya hiyo
iliyofanyika hivi karibuni mjini Arusha, lililojengwa kwa thamani ya shilingi
za Kitanzania Bilioni 26, zikiwa ni sehemu ya bilioni 30 zilizotolewa kama ufadhili wa serikali ya Ujerumani kwenye jumuiya
hiyo.
Rais
Kibaki anatarajiwa kumkabidhi Rais Yoweri Museveni uenyekiti wa Marais wa nchi
tano za jumuiya katika mkutano wa mwaka wa viongozi hao utakaoanza hivi
karibuni jijini Nairobi nchini Kenya .
Kiongozi
huyo wa Kenya ambaye
amesisitiza umoja wa wananchi wa nchi zote tano za jumuiya ya Afrika Mashariki,
anatarajiwa pia kuachia rasmi, Urais wa Kenya
mwezi wa tatu mwakani baada ya uchaguzi utakaomsimika kiongozi mpya wa taifa hilo .
"Jumuiya
yetu imepanuka kutoka kwenye uanachama wa nchi tatu hadi tano za sasa, na jengo
hili ndiyo kielelezo cha umoja wetu," alisema Kibaki katika uzinduzi huo
wa majengo mapya ya makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mapema
akilihutubia bunge la Afrika Mashariki, Rais Jakaya Kikwete alitahadharisha
kuwa Jumuiya hiyo isikimbilie kwenye umoja wa sarafu kabla kwanza kufanya
utafiti wa kutosha juu ya jambo hilo .
Aidha wakuu wa nchi za jumuia ya afrika mashariki, (EAC).hivi
karibuni walizindua rasmi majengo mapya
ya makao makuu ya jumuia hiyo yaliyopo mjini Arusha ambapo Katika hafla hiyo fupi,
Marais 5 walishiriki katika uzinduzi huo.
Uzinduzi huo unaiwezesha jumuia hiyo kuwa na majengo yake
tangia izinduliwe kwa mara ya pili mwaka 1998 ,ambapo awali ilikuwa imepanga
katika majengo ya kituo cha mikutano ya kimataifa AICC.
0 comments:
Post a Comment