Gari
ndogo yenye nambari za usajili Z 897 DF ikionekana kuvurugika kabisa
baada ya kifusi cha dari ya jengo la Makumbusho ya Taifa la Beit al
ajaib kuidondokea kufuatia mvua za vuli zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
Sehemu
ya jengo la Makumbusho ya Taifa la Beit Al Ajaib ikionekana kunyofuka
kutokana na mvua za vuli zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia sehemu ya
jingo la beit al ajaib ambayo imebomoka kutokana na mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akijaribu kuchungulia baadhi ya sehemu ya Jengo la
Makumbusho ya Taifa ambalo nyuma ya jengo hilo limepata maafa ya
kubomoka.
Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk.
Na Othman Khamis Ame OMPR
Wakati neema ya mvua za vuli ikiendelea kunawiri katika maeneo mbali mbali nchini ikileta faraja zaidi
kwa wakulima na wafugaji kwa kupata malisho ya Mifugo yao lakini kwa
upande mwengine mvua hiyo hiyo imeonekana kuleta hasara.
Hasara hiyo
inaonekana kuikumba Wizara ya Habari,Utamaduni, Utalii na Michezo
kufuatia Jengo lake Maarufu la Makumbusho ya Taifa la Beit Al- Ajaib
liliopo Forodhani Mjini Zanzibar kubomoka upande wa nyuma wa Jengo hilo.
Kifusi kilichodondoka kutoka kwenye Dari ya Jengo hilo robo yake kimeishia kwenye
gari moja ndogo yenye nambari za usajili Z 897 DF inayomilikiwa na
Bwana Said Saleh Saidi Mkaazi wa Forodhani ambae alikuwa ameiegesha
pembezoni mwa Jengo hilo.
0 comments:
Post a Comment