Wafuasi
wa rais huyo wameharibu mahema yaliyowekwa nje ya ikulu hiyo na
wapinzani wa Morsi walioanza kukesha nje ya ikulu hiyo Jumanne kupinga
mamlaka aliyojilimbikizia
Pia wanapinga rasimu ya katiba mpya ambayo itapigiwa kura ya maoni tarehe 15 mwezi Disemba
Makamu wa rais Mahmoud Mekky,amesema kuwa mabadiliko yaliyofanyiwa katiba hiyo yanaweza kukubalika na upinzani.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton amesema mazungumzo yanahitajika haraka kuhusu katiba hiyo.
Maelfu ya wapinzani wa rais wameapa kuendelea na maandamano yao nje ya ikulu ya rais mjini Cairo.
Baadhi wameweka mahema nje ya ikulu na sasa wanuzunguka ukuta wa ikulu hiyo.
Siku
ya Jumanne , maelfu ya waandamanaji walivamia ikulu wakipinga rasimu ya
katiba iliyozua utata mkubwa pamoja na kupinga sheria inayomlimbikizia
mamlaka makuu Rais Morsi.
Wakati mmoja polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao ambao walikuwa wamevuka ukuta wa seng'enge.
Vikosi vya usalama vilitoa taarifa vikisema kuwa rais Morsi ameondoka katika ikulu hiyo na ameomba utulivu.
Waandamanaji hao wanapinga hatua ya rais kujilimbikizia madaraka mapya na kusababisha kuundwa kwa rasimu ya Katiba.
chanzo:bbc
0 comments:
Post a Comment