Rais
Jakaya Kikwete (pichani) amewataka Watanzania kujivunia na kuyaenzi
mafanikio ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, yaliyopatikana tangu nchi
ilipojipatia uhuru wake mwaka 1961.
Akizungumza
katika maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara, uliofanyika
kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salam leo, Rais Kikwete alisema
yamekuwa tofauti na ya awali, safari hii yakihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa kuu kutoka nchi 14 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC).
Alisema mafanikio hayo yametokana na uvumilivu wa kisiasa ujengeka miongoni mwa Watanzania.
Viongozi
mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph
Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa
Msumbiji Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa
awamu ya pili
Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa na Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja
wa Taifa.
Kikwete
alisema katika miaka 51 ya uhuru wa nchi hiyo, imekuwa katika utulivu
na amani ambapo utulivu huo umekuwa chachu ya maendeleo katika jamii ya
Watanzania.
Aidha,
viongozi waliohudhuria maadhimisho hayo, Rais Kikwete amewataja kuwa ni
pamoja Rais wa Jamhuri ya Congo (DRC), Joseph Kabange Kabila, Emilio
Armando Guebuza, (Msumbiji), na Hifikepunye Pohamba (Namibia), mbaye
alishuhudia Tanzania Bara ikipata uhuru mwaka 1961 na Makamu wa Rais wa
Zambia Guy Scott.
Wengine
ni Makamu wa Rais wa Angola Manuel Domingos, Waziri Mkuu wa Rwanda,
Pierre Au Moyen, Waziri Mukuu wa Swazland, Sibusiso Dlamini, Simba
rashe na wengine.
Katika
sherehe za maadhimisho hayo kulikuwa na burudani mbalimbali ikiwemo
gweride la vikosi vya Majeshi, Halaiki ya watoto na ngoma za asili
pamoja na kikundi cha Taifa cha ngoma za asili kutoka Rwanda.
0 comments:
Post a Comment