Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Katika
kile kinachoonekana kuhamasisha madereva wa pikipiki za abiria maarufu
kama boda boda kupata mafunzo yao kupitia vyuo, jeshi la Polisi mkoa wa
Arusha kupitia kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na baadhi
ya vyuo vya udereva wameanza kutoa mafunzo kupitia ofisi za kata.
Neema
hiyo ilitangazwa juzi kwa Madereva hao na Mkuu wa Kikosi hicho Mkoa wa
Arusha Mrakibu wa Polisi Harison Mwakyoma alipokuwa anazungumza nao
katika mkutano uliofanyika kiwanja cha kata Kimandolu.
Alisema
kwamba ameamua kuongea na baadhi ya wamiliki wa vyuo vya udereva
vilivyopo mkoani hapa ili watoe mafunzo hayo kwa madereva kwenye kata
zao tena kwa gharama ya chini Kabisa ambayo ni Tsh 30,000 tu hali ambayo itasaidia
kutoa hamasa kubwa kwa madereva hao kujifunza.
“Pamoja
na kujua kuendesha pikipiki ila hamjui sheria za usalama barabarani,
mafunzo yatawasaidia sana, mbali na kujua sheria za usalama barabarani
ambazo zitawasaidia kuepusha ajali pia yatawasaidia kujua haki zenu”. Alisema Mwakyoma.
Aliongeza
kwa kuwaambia kuwa siku zote wakitaka wasifuatiliwe na askari
wanatakiwa wawe wametimiza vigezo vyote wanapokuwa barabarani kama vile
kuwa na leseni ya udereva, kofia ngumu “Helmet” n.k.
Mkuu
huyo wa Usalama barabarani amesema ameanzisha kampeni hiyo ili kila
mmoja apate mafunzo yake kupitia chuo hali ambayo itasaidia kupunguza
ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa.
Mkutano
huo uliohudhuriwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi
Gilles Muroto, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi toka Dawati la Jinsia na
Watoto, Maria Maswa, Polisi tarafa, viongozi wa tarafa ya Suye, kata,
mitaa na madereva wapatao 100.
Mkutano huo pia ulitawaliwa na makofi ya pongezi pamoja
na vifijo kutoka kwa madeva hao baada ya Mkuu huyo wa Usalama
Barabarani kuwaahidi kuwa kama wangekuwa tayari hata siku ya pili yake
(jana) wangeweza kuanza darasa.
Alimalizia
kwa kuwaasa madereva hao kutojichukulia sheria mkononi pindi mwenzao
anapogongwa na gari kwani vitendo hivyo vinaweza kuwagharimu badala
yake aliwataka wafanye mambo manne muhimu; kwanza kuandika namba ya
gari iliyosababisha ajali, kuielewa mahali ajali ilipotokea, kutoa
taarifa polisi na mwisho kumwahisha mwenzao hospitali.
Programu
ya mafunzo kwa waendesha pikipiki mkoani hapa ilianza rasmi mwezi
Agosti mwaka huu baada ya kufunguliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas kutokana na kuwepo
kwa ongezeko kubwa la ajali.
Hali
hiyo imesaidia sana kupunguza kiwango cha ajali mkoani hapa toka
wastani wa ajali 5 za boda boda kwa wiki hadi moja au kutokuwepo kabisa.
Hadi
sasa waendesha boda boda wapatao 900 kutoka wilaya za Arusha mjini,
Arumeru na Monduli wamekwisha pata mafunzo ya udereva toka vyuo
mbalimbali vilivyopo mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment