270 wafariki katika kimbunga Ufilipino
Wengine wengi
hawajulikani waliko. Nusu ya walioathiriwa walikuwa ni wakaazi katika
maeneo ya milima walioathirika na maporomoka ya udongo baada ya
kuyakimbia makaazi yao ili kwenda kwenye maeneo yalio salama.
Katibu
mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo, Gwendolin Paang,
ameiambia BBC kuwa idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka shirika la AP Miili zaidi ya 270 ya watu
waliofariki katika kimbunga hicho ilipokelewa katika maeneo
yalioathiriwa na kimbunga hicho kusini mwa ufilipino.
Kwa
mujibu wa maafisa nchini humo huenda miili zaidi ikapatikana katika
maeneo mengine ambayo kwa sasa waokoaji wanaendeleza shughuli za uokozi.
Katika
mkoa wa Compostela zaidi ya watu 151 wakiwemo wanajeshi na wenyeji
wameripotiwa kufariki katika mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga
hichi cha bopha .
Zaidi ya watu 80 waliponea kimbunga hicho lakini wengi bado hawajulikani walipo na wengine zaidi ya elfu 45 wakikosa makao.
Idadi
ya vifo hivi vimetokea licha ya rais wa ufilipino Benigno Aquino kutaka
raia wa ufilipino kuhamia maeneo yaliyo salama. Nchi ya ufilipino
hukumbwa na zaidi ya vimbunga 20 kila mwaka.
.........XXX............XXX............XXX...........
Wanajeshi 12 wa Somalia wauawa na Al Shabaab
Maafisa
kutoka jimbo lililojitenga la Puntland nchini Somalia wamesema kuwa
wanajeshi kumi na mbili wa serikali ya Somalia wameuwawa na kundi la
wanamgambo wa kislaamu la Al shabaab katika eneo la milima ya Galgalo
Walisema kulikuwa na mashambulizi mawili tofautio ambapo wanjeshi waliuawa katika eneo la milimani la Galgalo.
Kwa mujibu wa taarifa za kundi la Al shabaab waliwauawa zaidi ya wanajeshi 30 wa serikali kabla kutoweka katika milima hiyo.
Wapiganaji
wengi wa Al Shabaab wameripotiwa kukimbilia eneo la Puntland katika
miezi ya hivi karibuni huku jeshi la Somalia pamoja na wanajeshi wa
Muungano wa Afrika kudhibiti Kusini mwa Somalia.
chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment