Imeeleza kuwa changamoto inayoikabili jiji la Arusha la
ukosefu wa maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya viwanda ndio
chanzo kinachowafanya wawekezaji wengi kulimbikiza uwekezaji wao katika
mahoteli peke yake na kuacha fursa nyingi zikidorora.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa bodi ya viwanda na biashara (TCCIA) ambaye pia ni
mkurugenzi wa kiwanda cha banana investment ltd, Adolf R. Olomi alipokuwa
akizungumza na gazeti hili juu ya fursa za uwekezaji hasa katika sekta ya
viwanda.
baadhi ya waandishi wa habari mkoani Arusha wakipatiwa maelekezo ndani ya kiwanda hicho cha banana na mkurugenzi huyo bwana Olomi ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao ya biashara |
Olomi alisema kuwa hapa mkoani Arusha hasa hapa jijini kuna
fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo viwanda, biashara, ujasiriamali hasa wa
viwanda vidogo chini ya SIDO, pamoja na utalii ambazo zinaweza kuipatia mkoa
mapato mengi itakayosaidia kupangia bajeti zake za kimaendeleo.
Alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa fursa hizo lakini
changamoto kubwa ya jiji letu la Arusha kushindwa
kutenga maeneo maalum kwa ajili ya viwanda
kwa muda mrefu sasa, imesababisha watu wengi kutoona fursa hizo za uwekezaji na
matokeo yake wengi hukimbilia kuwekeza katika utalii kwa kujenga mahoteli ya kulala wageni kwa wingi.
“Simaanishi kuwa watu kuwekeza katika hoteli ni mbaya laa,
hasha…! kwani inatupatia mapato ya kufanyia shughuli za maendeleo hivyo hata niwakaribishe
na wengine waendelee kuja kuwekeza zaidi kutoka ndani na nje ya nchi, ila mimi
ninachopendekeza wawekeze katika maeneo mengine tofauti tofauti ikiwemo kilimo,
ujasiriamali, madini, miundombinu n.k.” alisema Olomi
ndani ya kiwanda cha banana, uzalishaji mvinyo ukiendelea |
baadhi ya wafanyakazi katika kianda hicho cha Banana wakianza kupanga chupa tayari kuwekwa kwenye kreti zake kuingia sokoni baada ya uzalishaji |
Akitolea mfano kiwanda chake cha kutengeneza mvinyo wa aina
mbalimbali kwa kutumia ndizi, Olomi anasema “kwa mfano mimi pamoja na kuwekeza
katika kiwanda nimewawezesha wakulima wa ndizi kuwa na soko la uhakika wa kuuza
ndizi zao hasa wanaotoka Meru na Moshi ambako kila siku tunatumia tani tano za
ndizi kutoka kwao”.
Aidha alisema kuwa kutokana na jiji kutotenga maeneo maalum
kwa ajili ya viwanda, amekuwa akipata kero nyingi kutoka kwa wakazi wa eneo
hilo alilojenga kiwanda chake kwani kwa sasa kiwanda hicho kimezungukwa na
makazi ya watu hivyo hutuhumiwa kila siku kwa mamba mbali mbali ikiwemo kelele
zitokanazo na mashine, pia moshi wa mashine, n.k.
Akijibu swali la riba zinazotozwa na taasisi za fedha katika
mikopo zinavyowagharimu Olomi anasema “Kiukweli hizi riba zinatuumiza wengi
kwani imekuwa tunawanufaisha wamiliki na kwa kutumia nguvu nyingi kurejesha
mkopo hali ambayo inachelewesha maendeleo ya muhusika……, kwa mfano mimi natumia
mikopo kuendesha shughuli zangu ambapo nakopa East Afrika development Bank(EADB)
na CRDB bank ambapo riba ni asilimia18 hadi22 hali ambayo inaniumiza sana hivyo
niwaombe wafanye hata 15%.
Kiwanda hicho cha banana kinatotengeneza mvinyo wa aina
mbalimbali ikiwemo fiesta, Raha Original, Raha poa pia wanatarajia kuwa
na aina zingine hivi karibuni aina za wine.
Mea wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo alipokuwa akitolea ufafanuzi changamoto hiyo ya ukosefu wa maeneo kwaajili ya viwanda |
Akijibu swala hilo la jiji la Arusha kukosa eneo maalum
kwaajili ya viwanda, Mea wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo alisema kuwa “ ni
kweli awali hakukuwa na meneo maalum kwa ajili ya viwanda lakini kwa sasa
wameshatenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambapo hata hivyo
hakuweza kubainisha ukubwa wake.
Alizitaja kata ambazo kuna maeneo hayo yaliyotengwa kwa
ajili ya viwanda kuwa ni pamoja na Moshono, Terrat, Olasiti ambapo tathmini
yamekwisha fanyika kwaajili ya kuwafidia wahusika walioko maeneo hayo kwa
kutumia faedha za world bank.
Lyimo pia alisema kuwa bado maeneo hayo hayajarihirishwa kwa
watu kutokana na bado liko kwenya maboresho hivyo itakavyokamilika wataangaza
baada ya kuweka mpango kabambe wa master plan ya jiji ambapo pia watatangaza
maeneo hayo yana ukubwa gain.
0 comments:
Post a Comment