mwenyekiti wa taifa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Freeman
Mbowe akisalimiana na laira Odiga huko nchini kenya.
MAHASIMU wawili wa kisiasa nchini Kenya, Raila Odinga na Uhuru
Kenyatta, wameingia katika mpambano wa kugombea urais nchini humo baada
ya kila mmoja kupitishwa na muungano wa vyama vyao.
Raila
ni Waziri Mkuu katika Serikali inayomaliza muda wake chini ya Rais Mwai
Kibaki wakati Kenyatta ni Naibu Waziri Mkuu akimsaidia Raila.
Kenyatta alizindua kampeni zake mjini Mombasa, wakati Raila alikuwa mjini Nairobi na kila mmoja aliwaambia wafuasi wake kwamba anahitaji kupambana na ukabila na kujenga mshikamano wa wananchi wote wa Kenya.
Kenyatta alizindua kampeni zake mjini Mombasa, wakati Raila alikuwa mjini Nairobi na kila mmoja aliwaambia wafuasi wake kwamba anahitaji kupambana na ukabila na kujenga mshikamano wa wananchi wote wa Kenya.
Mudavadi hakufanikiwa kupewa hata fursa ya kuwa mgombea mwenza wa Kenyatta na badala yake nafasi hiyo amepewa William Ruto.
Kwa upande wa Muungano wa Cord, wao walimpitisha Raila kugombea akiwa na mgombea mwenza, Steven Kalonzo Musyoka ambaye ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo hivi sasa.
Raila alieleza kuwa atawaondolea Wakenya matatizo ya ajira na lindi la umaskini, hivyo aliwasihi kuunga mkono Muungano wa Cord ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake, Kenyatta alisema Wakenya wameteseka kwa muda mrefu na sasa ameamua kujituma ili kuwakwamua katika lindi la umaskini na shida.
0 comments:
Post a Comment